Mke wa
Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwa amewabeba watoto, Editha
(kushoto) na Edina wa Kituo cha kulea watoto yatima cha CHAKUWAMA
kilichopo Sinza jijini Dae es salaam jijini Dar es salaam wakati
alipotembelea kituo hicho na kutoa misaada mbalimbali. Desemba 24, 201.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MKE wa
Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa
makundi ya watoto yatima jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha kufurahia
sikukuu za mwisho wa mwaka.
Mama
Majaliwa ametoa msaada huo leo (Jumamosi, Desemba 24, 2016) katika vituo
vitatu vya CHAKUWAMA kilichopo Sinza, HISANI kilichopo Kigamboni na
CHAMAZI kilichopo Mbagala.
Akikabidhi
msaada huo ikiwemo mchele, sabuni, mbuzi, juisi na soda, Mama Majaliwa
amesema ameona ni vema atoe msaada huo kwa watoto hao ili na wao waweze
kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka kama ilivyo kwa watoto wengine.
Pia ametoa mwito kwa makundi mbalimbali yenye uwezo katika jamii wawe na moyo wa kusaidia makundi yenye uhitaji.
Kwa
upande wao, walezi wa vituo vya kulelea watoto yatima vya CHAKUWAMA na
HISANI wamemshukuru mke wa Waziri Mkuu kwa msaada huo huku baadhi ya
watoto wakisema msaada huo umewapa faraja kubwa.
Mlezi wa
kituo cha CHAKUWAMA, Bibi Saida Hassan mbali ya kushukuru kwa msaada
huo, amewaombea kwa Mwenyezi Mungu awape afya na nguvu za kuendelea
kuwatumikia vizuri Watanzania.
Naye
Mlezi wa kituo cha HISANI, Bi. Hidaya Mutalemwa ameiomba jamii iendelee
kuyakumbuka makundi yenye uhitaji kwani bado yanakabiliwa na changamoto
nyingi za kufanikisha ndoto zao ikiwemo kupata elimu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269