Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa Kampuni ya The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku nyumbani, Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam leo. alipofika katika shughuli ya kuaga mwili wa Bukuku ambaye anatarajiwa kuzikwa kesho Desemba 27, 2016, katika makaburi ya familia yaliyopo Msalato, nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Nape akiwa na waombolezaji nyumbani kwa marehemu, Tabata Kimanga.
Wanafamilia.
Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akimpa pole mjane wa marehemu, Lilian Mpoki alipoenda kuifariji familia hiyo na kushiriki katika shughuli ya kuaga mwili.
Baadhi ya jamaa na marafiki wa marehemu Mpoki Bukuku wakiwa nyumbani wakati wa maandalizi ya kuaga mwili leo.
Mkurugenzi wa Radio One, Deo Rweyunga akisalimiana na Mwandishi wa siku nyingi, Said Msonda. Kulia ni mwandishi wa Habari leo Nelson Goima.
Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye (kulia) akisaidia kubeba jeneza.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye na Mhariri Mtendaji wa New Habari (kulia), Absalom Kibanda wakienda kwenye eneo la kuagia mwili.
Waombolezaji wakiwasili na jeneza katika viwanja vya Shule ya Sekondari Wazazi Tabata Kimanga kwa ajili ya kuaga nwili.
Ndugu wa marehemu wakiwasili katika eneo la kuaga mwili.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisalimiana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye alipowasili kuaga mwili wa marehemu Bukuku.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisalimiana na Mbunge wa Ubungo, Sayed Kubenea.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye wakifurahia jambo baada ya kuteta wakati wakisubiri kuaga mwili.
Baadhi ya waombolezaji.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269