Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole
Bi Mugwe Mbabe ambaye ni Mke mkubwa wa Marehemu Mzee Maarufu
Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa
marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi.
Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82)
Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Deodatus Manyama wakwanza (kushoto) ambaye ni mdogo wa marehemu Marehemu
Mzee Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa
Marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Bi. Mugwe Mbabe mke mkubwa wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama
mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini
daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee
Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini
daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee
Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
kutoa pole katika msiba huo wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama
mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Chato mkoani Geita
Mdogo wa
Marehemu Deodatus Manyama kimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara
baada ya kuwapa pole na kuwafariji kufuatia msiba wa Mpendwa wao
Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafiwa katika msiba huo Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafiwa katika msiba huo Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka msibani mara baada ya kutoa pole. PICHA NA IKULU.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29
Desemba, 2016 ameungana na wananchi wenzake Wilayani Chato mkoani Geita
kutoa pole kutokana na kifo cha Mzee Admirabilis Mbabe Manyama ambaye ni
mzee maarufu wilayani hapa na Mzee James Lufunga Mchele ambaye ni
jirani yake.
Rais
Magufuli pamoja na kuwapa pole wafiwa na wananchi wa Chato kwa
kuondokewa na mpendwa wao pia amitaka familia ya mzee Manyama kuendelea
kuishi kwa kushikamana na kupendana kama ilivyokuwa enzi za uhai wa
marehemu na kuwataka kuepukana na mifarakano.
”Unapotokea
msiba kama huu katika familia nyingi huzuka mifarakano, ombi langu
kwenu wewe Mama mkubwa na Mama mdogo kamwe msikubali kufarakanishwa
kutokana na kifo cha mume wenu,muwaongoze watoto wenu ili muendelee
kuishi kwa kupendana kama enzi za uhai wa mzee”
Aidha
Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Mzee Manyama kuwa alikuwa mzee
maarufu kijijini hapa na miongoni mwa mafundi hodari wa kushona nguo
ambaye pia alimshonea sare zake za shule wakati akisoma.
Kwa
upande wake Mdogo wa marehemu ambaye ni msemaji wa familia Bwana
Deodatus Manyama ambaye ni msemaji wa familia amemshukuru Rais Magufuli
pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kuwapa pole katika msiba huo, na
kwamba kitendo hicho kinaonyesha kuwa Rais magufuli si mtu asiejikweza
wala asiye na majivuno.
Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama amefariki akiwa na umri wa miaka 80,ameacha wajane wawili,watoto 15 na wajukuuu kadhaa.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato, Geita.
29 Desemba, 2016(P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269