.

RAIS WA GAMBIA ATUHUMIWA KUFANYA MAGENDO

Dec 18, 2016

Rais Yahya Jammeh wa Gambia
Gazeti la Le Monde la nchini Ufaransa limefichua kuwa, Rais Yahya Jammeh wa Gambia anatumia ndege yake binafsi kufanya magendo ya silaha na vitui vingine katika kona mbalimbali za dunia.
Gazeti hilo limeandika hayo katika toleo lake la leo Jumapili na kuwanukuu maafisa wa uwanja  wa ndege wa Gambia wakisema kuwa, Jammeh ambaye ameitawala nchini hiyo  ya magharibi mwa Afrika kwa zaidi ya miaka 22 kabla ya kushindwa kwenye uchaguzi wa hivi karibuni, anatumia ndege yake binafsi kufanya magendo kama vile ya silaha, mihadarati na almasi.
Wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Banjul, mji mkuu wa Gambia wamenukuliwa na gazeti la hilo la Ufaransa wakisema kuwa, wameshuhudia ndege binafsi ya Yahya Jammeh ikisafirisha bidhaa kwa siri nyakati za usiku na hakuna mtu yeyote aliyethubutu kupekua mizigo au wasafiri wa ndege hiyo.

Mwaka 2001 pia, kundi moja la wachunguzi wa Umoja wa Mataifa ambao walitumwa kufanya uchunguzi kuhusu matukio ya Liberia walisema wana wasiwasi ndege binafsi ya Rais Yahya Jammeh wa Gambia ilitumika kumtumia silaha Charles Taylor, rais wa zamani wa Liberia.. Ikumbukwe kuwa mwaka 2012, Taylor alihukumiwa kifungo cha miaka 50 jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya jinai dhidi ya binadamu nchini Liberia.
Habari kuhusu magendo hayo yanayodaiwa kufanywa na Rais wa Gambia zimesambazwa wakati huu ambapo Yahya Jammeh amekataa matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi mpinzani wake. Hadi hivi sasa viongozi wa nchi za Afrika wameshindwa kumshawishi Yahya Jammeh aachie madaraka kwa amani.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช