.

WATU SITA WAUAWA KATIKA SHAMBULIO LA KIGAIDI SOMALIA

Dec 28, 2016

Watu sita wameuawa katika shambulio lililofanywa leo na wanamgambo wenye mfungamano na kundi la kigaidi la al Shabab.
Tovuti ya habari ya All Africa imeripoti kuwa, watu sita wameuawa katika shambulio lililofanywa leo na watu wenye silaha wenye mfungamano na kundi la al Shabab katikati mwa Somalia. 
Wanamgambo wa al Shabab wenye makao yao Somalia 
Kundi la al Shabab hivi sasa limezidisha vitisho vyake katika maeneo mbalimbali ya Somalia;  na kusababisha kwa mara kadhaa kuakhirishwa uchaguzi mkuu nchini humo. Wakati huo huo, magaidi wa al Shabab wanaendelea kushikilia baadhi ya miji na vijiji vya Somalia huku wakiendesha mashambulizi dhidi ya vituo vya jeshi, vikosi vya serikali na vya Umoja wa Afrika.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช