Breaking News

Your Ad Spot

Jan 20, 2017

DK. MPANGO AZINDUA JINA NA NEMBO MPYA YA KIBIASHARA YA BENKI YA POSTA TANZANIA (Tpb Bank Plc)

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akibonyeza kitufe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa Jina Jipya na Nembo Mpya yenye alama ya Kipepeo, (Tpb Bank Plc) vitakavyo tumiwa kibiashara na Benki ya Posta Tanzania Plc. Tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Prof. Lettice Rutashobya na Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi, wakiangalia Jina Jipya na Nembo Mpya iliyobuniwa na Benki hiyo baada ya kuizindua rasmi  Jana, Tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (wa pili kulia), akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Bw. Sabasaba Moshingi, kwa kazi nzuri ambayo benki hiyo imefanya kubuni Jina na Nembo Mpya itakayoanza kuitambulisha Benki hiyo katika biashara ya Sekta ya Fedha, tukio lililofanyika katika ukumbi...
wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam

 Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Bw. Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba ya mafanikio ambayo Benki yake imeyapata katika biashara ya Sekta ya Fedha ikiwemo kukuza mtaji, kupata faida na kufanikiwa kubuni Jina Jipya na Nembo Mpya ya Kipepeo, itakayoanza kutumika kuanzia jana 19, 2017, baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akitoa hotuba kabla ya kuzindua rasmi Jina Jipya na Nembo vitakavyo tumiwa kibiashara na Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), kuanzia  Jna 19, 2017. Tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (aliyeketi kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tpb Bank Plc, Prof. Lettice Rutashobya (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Serkali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Khamis Juma, wakisikiliza kwa makini hotuba ama wasilisho la Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Sabasaba Moshingi, (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Jina na Nembo Mpya itakayoanza kuitambulisha Benki hiyo katika biashara ya Sekta ya Fedha kuanzia Jana 19, 2017, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tpb Bank Plc, Prof. Lettice Rutashobya (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, zawadi ya saa yenye Jina na Nembo Mpya ya Kipepeo, itakayoanza kuitambulisha rasmi Benki hiyo ndani na nje ya nchi baada ya kuzinduliwa rasmi kwa matumizi ya vitu hivyo, , tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tpb Bank Plc, Prof. Lettice Rutashobya (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, kadi ya benki hiyo mara baada ya kuzinduliwa kwa Jina na Nembo Mpya ya Kipepeo, itakayoanza kuitambulisha rasmi Benki hiyo ndani na nje ya nchi kuanzia jana, Tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
 Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, ambapo tukio la uzinduzi wa Jina na Nembo Mpya ya Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc) limefanyika.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt, Philip Mpango, (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Prof Lettice Rutashobya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Serkali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Khamis Juma, (wa kwanza kushoto), Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Sabasaba Moshingi (kulia), na Baadhi ya Watendaji wakuu wa Benki hiyo, baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Jina na Nembo Mpya ya Benki hiyo, Katika Ukumbi wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt, Philip Mpango, (wa pili kulia) akiwa  katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Prof Lettice Rutashobya, (wa tatu kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Serkali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Khamis Juma, (wa kwanza kushoto), Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Sabasaba Moshingi (kulia), na baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo, baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Jina na Nembo Mpya ya Benki hiyo, Katika Ukumbi wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt, Philip Mpango, (wa pili kulia) akiwa  katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Prof Lettice Rutashobya, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (wa kwanza kushoto), Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw, Sabasaba Moshingi (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wanawake wa  Benki hiyo baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Jina na Nembo Mpya ya Benki hiyo, Katika Ukumbi wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, jana (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages