Breaking News

Your Ad Spot

Jul 14, 2017

ROONEY, EVATON WAFURAHIA UKARIMU WA WATANZANIA

Wayne Rooney (wapili kushoto) kushoto akiwa na wachezaji wenzake walipokuwa Jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Everton ilicheza na timu ya Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki ulichezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu-MAELEZO
Timu ya Soka ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uiungereza imemaliza ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania na kuelezwa kufurahishwa na namna Watanzania walivyoipokea timu hiyo.

Timu ya Everton iliwasili Tanzania siku ya Jumatano wiki hii ambapo jana ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.

“Imekuwa ni uzoefu mpya kwangu kuja hapa (Tanzania) na nina tumaini sasa Makamu wa Rais atakuwa akiishabikia Everton”, alieleza Wayne Rooney kupitia tovuti ya timu hiyo.

Pia katika akaunti yake ya mtandao wa tweeter, Rooney aliwashukuru washabikji wa Tanzania kwa kuiunga mkono Everton katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.

 “Great start to the pre-season. Special thanks to the fans supporting us in Tanzania”, aliandika Rooney akitoa shukrani za pekee kwa washabiki wa Tanzania.

Kwa upande wa Kocha wa timu hiyo, Ronald Koeman alielezea kufarahia ziara ya kuja Tanzania na zaidi ni kutokana na hali ya urafiki iliyooneshwa na washabiki wa soka nchini.

Rooney pia aliungana na wachezaji wengine kama Morgan Schneiderlin, Jonjoe Kenny na Kevin Mirallas wa timu hiyo walipata fursa ya kujifunza tamaduni za kimsai, kujifunza kupika chakula cha asili, kutembelea shule yenye wanafunzi wenye mahutaji maalum na pia kufanya mazoezi na timu ya vijana wenye ulemavu wa ngozi (Albino United).

Timu ya soka ya Everton ilifanya ziara nchni Tanzania ambapo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, Marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na wageni mbalimbali kutoka ndani na nche ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages