Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo ameamua
kujiondoka kutoka chama tawala cha PDP, kinachotarajia kushiriki kwenye
uchaguzi march 28, na kuamua kuichana kadi yake ya uanachama hadharani.
Rais huyo wa zamani amekuwa mmoja ya wafuasi wa chama tawala cha PDP ambao wamekuwa wakimkosoa Rais Goodluck Jonathan, ambaye anawania awamu ya pili ya Urais wa nchi hiyo.
Obasanjo aliichana
kadi yake ya uanachama huku akiwaambia kwamba waichukue yeye haihitaji
tena kadi hiyo, hii haikupokelewa vizuri na inasemekana kuna mpasuko
ndani ya chama katika kipindi hiki cha mwisho wakati uchaguzi ukiwa
unakaribia.
Obasanjo amesema
kuwa hatojiunga na chama chochote atabaki kuwa raia wa kawaida na yuko
tayari kuchangia maendeleo ya taifa kwa kushirikiana na mtu yeyote bila
kujali msimamo wa kisiasa.
Rais Goodluck Jonathan amemlaumu Obasanjo kwa kukipigia debe chama kikuu cha upinzani All Progressives Congress (APC).
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269