NI
kama kumekucha! Siku chache tu baada ya Gazeti la Ijumaa (ndugu na
hili) kuandika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; Kiongozi wa
kikundi cha kigaidi kinachoua polisi na kuiba silaha kwenye vituo
nchini...NI HUYU, kundi jingine limeibuka na kuandika mkanda wa video
wakizungumzia uhalifu....
Cha
ajabu, sanjari na kundi hilo linalodai liko Tanga, Tanga hukohuko
kwenye Kitongoji cha Amboni, Ijumaa iliyopita kulizuka mapigano kati ya
polisi, askari wa JWTZ wakipambana na kundi lililodhaniwa ni la kigaidi
likiwa limepiga makazi ndani ya mapango ya kihistoria ya Amboni, Uwazi
lina full story.
Katika
mapigano hayo hadi juzi Jumapili, askari mmoja wa JWTZ aliuawa huku
wanajeshi watatu na askari polisi wawili wakijeruhiwa na kulazwa
Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo.
MASHUHUDA WA MAPIGANO
Kabla
Uwazi halijatiririka na video hiyo, lilizungumza na wananchi wenye
makazi yao kwenye Kitongoji cha Amboni ambako mapigano ya askari na
wahalifu yalitokea.
Mzee
Ibrahimu Ally, yeye anasema: “Siku ya tukio (Ijumaa asubuhi) mimi
nilikuwa nimepumzika ndani kwangu lakini ghafla nikasikia mlio wa risasi
kama mara mbili hivi.
“Mke
wangu alikuwa anafua, akaja mbio ndani akisema ni majambazi.
Nilimwambia funga mlango haraka sana, akaufunga. Lakini cha ajabu milio
ya risasi ikawa inaongezeka kadiri muda ulivyokwenda.
“Ilifika
mahali nikajua si majambazi bali tumevamiwa na majeshi ya nje ya nchi.
Kwani sasa risasi zilikuwa zikirindima kila muda. Hali ikawa tete kwa
kweli. Hata hapa ninapoongea na wewe siamini kama ile milio ya risasi
haitajirudia tena.”
WAZIKIMBIA NYUMBA
Mwanahawa
Mudale yeye alisema: “Ilibidi tuhame majumba kwenda kujificha, tatizo
ni ile milio ya mabomu na risasi na baadaye tukaona chopa (helikopta)
ikitembea angani. Awali tulijua ni vita ya nchi na nchi, kumbe walikuwa
askari wetu.”
SIKU MBILI HAKUNA KULALA
Baadhi
ya mashuhuda wanasema kutokana na milio ya risasi kwa siku ya Ijumaa
hadi Jumamosi asubuhi, hakuna mwananchi aliyepata usingizi.
“Mimi
na familia yangu hatujalala jamani. Risasi na mabomu yasikieni hivihivi
tu. Kuna wakati tulikuwa tukiona miale ya moto kutokea kwenye eneo la
mapango. Wakati mwingine badala ya moto tuliona moshi mkubwa.
“Kumbe wanajeshi wetu nao walishafika kupambana na hao watu,” alisema Simeon Patrick, mkazi wa Kitongoji cha Karasha, Amboni.
INAVYODAIWA
Habari
zilizosambaa juzi, zinadaiwa kundi hilo lililopambana na askari ni la
kigaidi ambapo safari yao kubwa ilikuwa kwenda kufanya ugaidi wa kumwaga
damu nchi jirani ya Kenya.
Wale jamaa nasikia walikuwa wakipeleka vifaa nchini Kenya eneo la mwambao ili waje wafanye uhalifu baadaye.
“Sasa
wakiwa katika hatua za mwisho mwisho baada ya kupeleka silaha za
kivita, wakashtukiwa. Ikabidi waache silala zao eneo walipozificha na
wao waje Tanga kujificha kwenye mapango.
“Lengo
lao, watulie mpaka hali kule Kenya itakapokuwa imepoa ndipo wajitokeze.
Sasa kilichotokea ni kwamba, wakati wanaishi mapangoni ilibidi waanze
kutoka kutafuta chakula kwa kufanya uhalifu mdogomdogo ndipo siku moja
jamaa yao mmoja akakamatwa kwa uhalifu.
“Yule
jamaa ndiye aliyewapeleka polisi walipo wenzake na kutokea kwa mapigano
makali kama yale,” alisema mtoa habari mmoja huku akiomba jina lake
lihifadhiwe.
WANACHOAMINI WANANCHI, TOFAUTI NA POLISI
Uwazi lilibahatika kuzungumza na baadhi ya wananchi wa jijini Tanga ambapo karibu wote walikuwa na mtazamo mmoja tu.
“Kutuambia
wale ni majambazi si sawasawa. Majambazi wetu tunawajua, polisi
wanawatosha sana, sasa hawa wametokea wapi mpaka JWTZ washirikishwe?”
alihoji Paulina Mathias, mkazi wa Chumbageni, Tanga.
Kusema
ukweli serikali ituambie moja. Lakini wale si majambazi. Kwanza mpaka
leo hii (juzi) hawajamkamata hata mmoja zaidi ya kujeruhi askari wetu na
kumuua mmoja. Wale ni magaidi, lazima tuwe makini sana,” alisema Ally,
mkazi wa Duga Maforoni, Tanga.
KUHUSU VIDEO MPYA
Tukiachana na mapigano ya Amboni, sasa turudi kwenye video mpya ya watu waliojiita ni watetezi wa haki dhidi ya udhalimu.
Video
hii ipo ndani ya mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wanaonekana watu
wawili wakiwa wamevaa mavazi ya kininja ili wasijulikane.
Watu
hao wanasema wanapinga jamii yao kukamatwa na kuuawa mara kwa mara
wakidai jeshi linawaonea hivyo kutangaza kupambana na askari.
Video hiyo haipishani sana na ile iliyotangulia kuandikwa kwenye gazeti ndugu na hili la Ijumaa.
KAULI YA JESHI LA POLISI
Akizungumza na Uwazi
jijini Tanga muda mfupi baada ya kutulia kwa mapambano ya Amboni,
Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja aliwataka
wananchi kutulia na kuendelea na shughuli zao za kawaida huku
akisisitiza:
“Askari walifika
mapangoni, kundi lile ni la majambazi. Lilianza kufanya mashambulizi ya
risasi na katika majibizano, askari sita walijeruhiwa na kuwahishwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo,” amesema Kamishna Chagonja.
~GPL
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269