Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Mizengo Kayanza Pinda anatarajiwa kufungua mkutano wa Nne wa Wadau wa
Mfuko wa Pensheni wa PSPF utakaofanyika tarehe 18 na 19 Februari 2015
katika Manispaa ya Dodoma. Kauli mbiu ya mkutano huo ni, ‘PSPF- chaguo
lako sahihi’.
Taarifa iliyotolewa na Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa
PSPF Bi. Costantina Martin, inasema mkutano huo ni mwendelezo wa
mikutano ya wadau inayofanyika kila mwaka kwa lengo la kupata fursa ya
kukutana na wadau wa Mfuko, kutoa taarifa ya mwaka ya Mfuko na kupokea
maoni na ushauri kwa ajili ya maendeleo ya Mfuko.
Katika mkutano huo PSPF itapata fursa ya kutambulisha kwa
wanachama na wadau Mkopo wa elimu na mkopo wa kuanza maisha, Bi. Martin
alisema; “mikopo hii hutolewa kwa wanachama wa PSPF wakiwa bado kazini
ili kutimiza malengo yao mbalimbali.
Meneja huyo alisema mafao mengine yanayotolewa na PSPF ni pamoja
na; mafao ya uzeeni, malipo ulemavu, malipo ya mirathi, rambirambi ya
mazishi, pensheni ya wategemezi, mafao ya kuachiswa kazi na fao la
kujitoa.
Pia alisema pamoja na kutoa mikopo ya elimu na mkopo wa kuanza
maisha, PSPF inatoa mikopo ya nyumba na mikopo kwa wastaafu yenye
masharti nafuu.
PSPF ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoanzishwa na sheria ya
Mafao ya Hitimisho la kazi kwa watumishi wa Umma namba 2 ya 1999 sura ya
371.
Your Ad Spot
Feb 17, 2015
Home
Unlabelled
Mhe. Pinda kufungua Mkutano wa Wadau wa PSPF
Mhe. Pinda kufungua Mkutano wa Wadau wa PSPF
Share This
About khamisimussa77@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269