Breaking News

Your Ad Spot

Feb 19, 2015

MWAKILISHI WA JIMBO LA MAGOMENI ZANZIBAR AFARIKI GHAFLA

salmin-awadhMwakilishi wa jimbo la Magomeni, Salmin Awadhi Salmin (pichani) amefariki dunia ghafla mchana huu akiwa mkutanoni katika ofisi kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.
Salmin Awadh ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  na Mnadhimu wa wajumbe wa CCM Baraza la Wawakilishi Zanzibar amefariki wakati akihudhuria vikao vya chama.

Marehemu Awadh alikimbizwa kwa matibabu Hospitali ya Mnazi Mmoja, Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages