MWIMBAJI wa kimataifa raia wa
Uingereza, Ayobami David ni mmoja wa waimbaji wanaopenekezwa sana na
mashabiki waalikwe katika onesho la miaka 15 ya Tamasha la Pasaka
nchini.
Ayobami ni mwimbaji ambaye anafanya vizuri katika muziki huo wa Kumtukuza Mungu kupitia nyimbo mbalimbali.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema katika taarifa yake
kuwa mwaka huu wanataka kutoka kivingine.
“Mashabiki wamekuwa wakiomba
tumualike Ayobami, bado tunapokea maoni mbalimbali na kulingana na
vigezo vyetu tutajipanga,” alisema Msama.
Alisema kwa kuwa wameamua kukuza
muziki huo hapa nchini, wataalika wasanii mbalimbali wa kimataifa ili
kulifanya tamasha la mwaka huu liwe la aina yake.
Alisema wamekuwa wakiwatumia
katika matamasha yake yaliyoasisiwa tangu mwaka 2000, waimbaji kutoka
Kenya, Zambia, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na
wa hapa nchini.
“Niliyoeleza mwanzoni
yanakamilika, kwa sababu nilidhamiria kuliboresha zaidi Tamasha la
Pasaka kwa kuwashirikisha waimbaji wa Kimataifa, mashabiki wakae mkao wa
kula kupata ladha tofauti katika tamasha la mwaka huu,” alisema Msama.
Baadhi ya waimbaji waliopata
kutumbuiza Tamasha la Pasaka tangu lianzishwe ni Rebecca Malope, Keke
Phoofolo (Afrika Kusini), Ephraim Sekereti (Zambia), Faraja Ntaboba
(DRC) na Sarah K, Paul Mwai (Kenya).
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269