Mshambuliaji machachari wa klabu ya
Yanga, ameiomba klabu yake kumlipia deni analodaiwa benki ili aweze
kucheza kwa bidii na kuwa mfungaji bora.
Ngasa aliamriwa kulipa deni la Sh 45
milioni kwa kosa la kujiunga na Yanga bila kufuata utaratibu akitokea
Simba, hivyo , kwa makubaliano, analazimika kukatwa Sh500,000 (wastani
wa dola 280) kila mwezi kutoka katika sehemu ya mshahara wake anaoupata
kutoka Yanga ili kulipa deni.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano
wa Yanga, Jerry Muro, benki , baada ya kukata 500,000, ililazimika
kuchukua mshahara wote wa Ngasa katika miezi ya hivi karibuni ili
kufidia deni analodaiwa baada ya uongozi uliopita wa klabu hiyo
kushindwa kupitisha benki mshahara wake benki kwa muda unaokisiwa mwaka
mmoja, hivyo kutolipa kwa mujibu wa makubaliano na benki kulazimika
kumuacha mchezaji huyo bila senti.
Ngasa aliripotiwa kusema kuwa hali yake
ya kifedha “financial status” ni mbaya na kushindwa kucheza vizuri, na
kuiomba Yanga kuangalia namna ya kumsaidia kulipa ili aweze kubakiwa na
fedha za kutoka.
“Tutakaa na Ngasa tuangalie namna ya kumsaidia”.
“Licha ya matatizo aliyonayo, ameonesha
kuwa ni mchezaji anayejituma na magoli mawili aliyofunga hivi karibuni
na kutupa ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika ligi kuu inaonesha
anavyoithamin i timu yake”, alisema Muro.
Kutokana na makato yanayomkabili, Ngasa,
ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu wa ligi, alitangaza
kuachana na Yanga ili akacheze mpira nje ya nchi, lakini klabu yake
imesema itamuongeza mkataba mwingine baada ya mazungumzo ya hivi
karibuni.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269