Breaking News

Your Ad Spot

Feb 10, 2015

MAALIM SEIF AWASILI MJINI DOHA, QATAR KWA ZIARA YA KISERIKALI

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Seif Sharif Hamad, akiwa na ujumbe wa SMZ mjini Doha kwa ajili ya kuanza ziara ya kiserikali nchini Qatar. 
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Awena Sinani Massoud (kushoto), akiwa na viongozi wengine wa SMZ tayari kwa kuanza ziara nchini Qatar.
Waziri wa Nchi, ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej, akibadilishana mawazo na maofisa wa mambo ya nje, tayari kwa kuanza ziara nchini Qatar. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Na Hassan Hamad, Doha, Qatar.
10/02/2015
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Seif Sharif Hamad, amewasili mjini Doha nchini Qatar kwa ajili ya ziara rasmi ya Kiserikali.

Katika ziara hiyo ya siku nne, Maalim Seif anaambatana na viongozi mbali mbali wa SMZ wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Ali Juma Shamuhuna na mwakilishi wa jimbo la Kwamtipura Mhe. Hamza Hassan Juma.

Viongozi wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr. Omar Dadi Shajak na Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, wanawake na watoto Bi. Asha Ali Abdallah.

Akiwa nchini Qatar, pamoja na mambo mengine Maalim Seif atatembelea mamlaka ya uwekezaji nchini humo pamoja na kuona na watanzania waishio nchini Qatar.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages