Rais Barack Obama
Rais
Barack Obama ameliomba baraza la Congress kupitisha mpango wa amiaka
mitatu wa mashambulizi dhidi ya kundi la wapiganaji wa Kiislam la
Islamic State ambalo linashikilia baadhi ya maeneo nchini Iraq. Mpango
huo wa Marekani dhidi ya wapiganaji wa IS unahusisha vikosi vya
mashambulizi ya ardhini katika jitihada za kutokomeza kundi hilo la
kigaidi. Hata hivyo Rais Obama amesema kuwa si kwamba anaomba idhini ya
kufanya mashambulizi hayo
kwani kwa mjibu wa mamlaka yake hakuna sheria inayoweza kumzuia na
kwamba hana nia ya kuendeleza mapigano nchini Iraq bali inamlazimu
kufanya hivyo kutokana na vitendo vya IS. Ni mara ya kwanza kwa Rais wa
Marekani kuomba idhini ya baraza la Congress ili kutumia majeshi yake
tangu utawala wa Rais George W Bush in 2002 pale alipoivamia Iraq
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269