RAIS
Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua
Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha
kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.
Akizungumza na waandishi wa habari
kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na
kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu
kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa
majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu
wa wilaya 12.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema,
Rais Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na
kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.
Wakuu wa Wilaya wapya 27
walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B.
Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu
anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick
Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging’ombe.
Wengine na vituo vyao kwenye
mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali
Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni),
Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S.
Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara
(Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen
Zelothe (Musoma).
Wengine ni Pili Moshi (Kwimba);
Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R.
Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui);
Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally
Mohamed (Serengeti).
Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi
wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali
Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa
Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa
Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa
Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).
Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa
Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri,
kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa
ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred
Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo
Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses
Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya
(Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias
Goroi (Rorya).
……………………………
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA. FEBRUARI 18, 2015.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269