Hii
ni ajali kubwa ya kwanza kutokea kwa mwaka 2015 ikihusisha vyombo vya
majini kupata ajali na kuua watu wengi ambapo zaidi ya wahamiaji 200
wamefariki baada boti mbili walizokuwa wakisafiria kuzama katika bahari
ya Mediterrania walipokuwa wakijaribu kuzamia kwenda Ulaya.
Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema ni watu nane pekee ndio waliweza kuokolewa baada ya kukaa majini kwa siku nne huku wengine 203 kutojulikana waliko.
Msemaji wa UNHCR Italia, Bi. Carlotta Sami aliandika
katika ukurasa wake wa Twitter kuwa boti mbili zilihusika katika ajali
hiyo na zilikuwa zikitokea Libya huku kila moja ikiwa na zaidi ya watu 100.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269