Mke wa Rais na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama
Salma Kikwete akiongea na viongozi wa CCM wa Tawi la Ufukoni katika Kata
ya Rahaleo huko Lindi Mjini tarehe 9.2.2015. Mama Salma Kikwete yupo
wilayani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku 5.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa
ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete
akikaribishwa na Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Lindi Mjini Dkt.
Zulfa Msami wakati Mama alipotembelea kituo hicho tarehe 10.2.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akimwangalia mtoto mwenye umri wa siku 2 aliyeshikwa na Mama yake
Sharifa Ali,19, wakiati Mama Salma alipotembelea kituo cha Afya cha
Lindi Mjini tarehe 10.2.2015.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa
anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwa amempakata mtoto
Adaita Hamis mwenye umri wa siku 1 aliyezaliwa katika Kituo cha Afya cha
Lindi Mjini tarehe 9.2.2015 huku akiongea na mama wa mtoto huyo Bibi
Zanida Ismail,42, anayeishi Mtaa wa Benki huko Lindi Mjini wakati Mama
Salma alitembelea kituoni hapo tarehe 10.2.2015.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269