Breaking News

Your Ad Spot

Feb 11, 2015

WIRAZA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MAKUBALIANO YA UJENZI WA WODI YA WATOTO NA WAZAZI.

EA1Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Mr. Jaap Frederiks akizungumza na baadhi ya watendaji wakuu wa Wizara ya Afya kabla ya utiaji saini makubaliano ya uboreshwaji wa wodi ya wazazi na watoto Unguja na Pemba, hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Zanzibar.
EA2Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Saleh M. Jidawi (wa kulia waliokaa) na Meneja wa Kampuni ya Simed International Services ya Uholanzi Nd. Michor Pleijzer wakitia saini mkataba wa uboreshwaji wa wodi ya wazazi na watoto Unguja na Pemba huku wakishuhudiwa na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Mr. Jaap Frederiks katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar). EA3 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Saleh M. Jidawi  (kulia)na Meneja wa Kampuni ya Simed International Services ya Uholanzi Nd. Michor Pleijzer wakibadilishana hati za makubaliano  ya uboreshwaji wodi ya wazazi na watoto za Unguja na Pemba katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar. EA4Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Mr. Jaap Frederiks (wakatikati mbele walio simama)katika picha ya pamoja ya viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman wa mbele kulia. Sherehe hiyo ilifanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
……………………………………………………………………………..
Na Abdulla Ali  Maelezo-Zanzibar    
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuokoa maisha ya Wanawake na Watoto kwa kuimarisha Miundombinu ya Afya.
Hayo ameyaeleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dr. Saleh M. Jidawi wakati akisaini Mkataba kwa ajili ya utekelezaji wa kuanza kwa mradi wa kuimarisha Afya za Mama na Watoto uliyofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo iliyopo Wilaya ya Mjini Unguja.
Mkataba huo uliosainiwa na Wizara ya Afya Zanzibar kupitia Katibu Mkuu Dr. Saleh M. Jidawi kwa pamoja na Meneja wa Kampuni ya Simed International ya Uholanzi Nd. Michor Pleijzier uliofanyika siku ya tarehe 11/02/2015 ni miongoni mwa muendelezo wa utekelezaji wa mradi huo ambao awali ulitiwa saini mnamo tarehe 23/12/2014.
Dr. jidawi amesema kuwa dhamira kuu ya mradi huo ni kuimarisha afya za kina mama na watoto waliozaliwa chini ya mwaka mmoja pamoja na kutoa huduma kwa watoto wengine.
Ametanabahisha kuwa utekelezaji wa mradi huo unakwenda sambamba na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2020 uliotafsiriwa na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA ii).
Amesema kuwa mradi huo unajumuisha maeneo mbalimbali ya utekelezaji ikiwemo upatikanaji wa vifaa, tiba, ukarabati wa vifaa, uboreshaji wa miundombinu pamoja na utoaji wa ushauri elekezi kwa Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Amesema sambamba na hayo mradi huo unakusudia kuviboresha vituo vya Afya 19 vya Unguja na Pemba ili vipate kutoa huduma bora kwa jamii.
Ametanabahisha kuwa kwa upande wa Hospitali ya Mnazi Mmoja mradi huo utajumuisha vitengo mbalimbali vikiwemo chumba cha upasuaji, maabara, duka la dawa, chumba cha wagonjwa mahututi cha watoto na wazazi, kitengo cha huduma za X-ray, wodi za wazazi, kitengo cha kutakasisha vifaa tiba, eneo maalumu la kuteketeza taka za hospitali pamoja na kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD).
Dr. Jidawi ameeleza kuwa mradi huo wa sekta ya Afya unaakisi maazimio ya Serikali zote mbili ambazo ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Uholanzi kwa kufanya kazi pamoja katika nyanja mbalimabali za kimaendeleo ikiwa ni pamoja na uchimabaji wa gesi, uhifadhi wa mwambao wa bahari, uendelezaji wa bandari pamoja na uhifadhi wa Mji Mkongwe.
Nae Balozi mdogo wa Uholanzi Nd. Jaap Frederiks ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuharakisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mradi huo na kazi iliyobakia ni kuanza rasmi kwa maazimio ya mradi huo ambao utachukua takriban Miezi 33 hadi kukamilika kwake.
Mradi huo utagharimu shilingi Bilioni 19.5 Tsh, ambapo asilimia 50% ya fedha hizo zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na 50% zilizobaki zimetolewa na Serikali ya Uholanzi, zaidi ya gharama hizo pia Serikali ya Uholanzi imetoa fedha kwa ajili ya uandaaji wa michoro pamoja na ushauri elekezi uliogharimu shilingi Milioni 720

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages