Kiungo
nyota wa Manchester United, Marouane Fellaini hatimaye ameamua kufunguka
na kuelezea alivyomwaga chozi baada ya kupata uhakika kocha David Moyes
alikuwa ametimuliwa kazi.
Fellaini
raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Uarabuni, amesema alishindwa kujizua na
kumwaga chozi baada ya kugundua kocha huyo kweli alikuwa amefukuzwa
kazi Aprili, mwaka jana.
“Nimefanya
kazi miaka sita na Moyes, kwangu alikuwa kama mzazi na alinisaidia
sana. Mimi ni binadamu, sikuwa na ujanja namachozi yalimwagika.
“Unajua nilisikia kwenye vyombo vya habari siku moja kabla lakini sikuwa na uhakika kama ni kweli au la.
“Siku
iliyofuata nilipofika mazoezini nilikwenda kwenye mgahawa, baadaye
nikamuona Moyes akiwa amevaa suti na si suti (trak suti), nikajua ni
kweli.
“Baadaye
alinifuata na kunichukua hadi ofisini kwake ambako kule alinieleza
ukweli kuhusiana na kuondoka kwake huku akinisisitiza huo ndiyo mpira
ulivyo, nililia,” anaeleza Fellaini.
Moyes
ndiye alimsajili Fellaini kutoka Everton ambayo aliifundisha kwa muda
mrefu zaidi na kumfanya kuwa kocha wa tatu kwa kudumu katika klabu moja
kwa muda mwingi nchini England baada ya Alex Ferguson na Manchester
United na Arsene Wenger na Arsenal.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269