Maafisa
nchini Rwanda wanasema kwamba baada ya mashauriano ya kitaifa ni watu
kumi tu wanaompinga rais Kagame kuwania muhula wa tatu.
Gazeti la
New Times lililo karibu na serikali linasema kati ya watu milioni mbili
walioshauriwa kuhusu kufanyia katiba mageuzi ni watu kumi tu waliopinga
fikra hiyo.
Katiba inasema rais anapaswa kuhudumu kwa mihula miwili pekee.
Wachambuzi wanasema raia wengi wa Rwanda huenda wameogopa kupinga pendekezo hilo.
Rais Kagame amehudumu madarakani tangu 1994.
(Taifa jirani la Burundi lilikumbwa na mgogoro mnamo mwezi Aprili baada ya rais Pierre Nkurunziza kuwania uhula wa tatu)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269