Ukisikia mpira wa wanaume ndio umepigwa usiku huu kati ya Mabingwa wa Ulaya, FC Barcelona na mabingwa wa Europa Ligi, Sevilla.
Timu hizo zimecheza fainali ya Uefa super Cup inayoashiria kufunguliwa rasmi kwa msimu mpya wa Ulaya.
Barcelona chini ya kocha Luis Enrique wameshinda 5-4 katika mchezo uliopigwa kwa dakika 120.
Dakika 90 zilimalizika kwa sare ya 4-4 ambapo magoli ya Barca yalifungwa na Lionel Messi (6, 16), Rafinha (42), Luis Suarez (54), huku ya Sevilla yakitiwa kambani na Ever Banega (3), Jose Antonio Reyes (57), Kevin Gameiro (72 penalti) na Yevheniy Konoplyanka (81).(VICTOR)
Dakika 30
za nyongeza wazee hao wa kazi waliendelea kutunishiana msuli, lakini
Pedro Rodriguez alimaliza kazi dakika ya 115 baada ya kuandika goli la
tano na la ushindi.
Barcelona wameanza msimu vizuri kwa kutwaa kombe lao la kwanza.
Pedro
amefunga goli hilo muhimu wakati huu akiwa katika rada za Manchester
United na baada ya mechi hii aliripotiwa kutimkia Old Trafford.
Msimu uliopita walitwaa makombe matatu (Treble) kwa maana ya La Liga, kombe la Mfalme na Uefa Champions Leagu.
Je, msimu huu watarudi rekodi hiyo?
Wachezaji
wa Barcelona wakisherehekea na taji lao na Super Cup ya UEFA walilotwaa
jana baada ya kuifunga mabao 5-4 mjini Tbilisi. Barca walimaliza msimu
uliopita wakishinda mataji matatu, Ligi ya Mabingwa, Kombe la Mfalme na
La Liga na wanafungua msimu vyema kwa taji la kwanza, Super Cup ya
Ulaya.
Wachezaji wa Barcelona wakishangilia taji lao la Super Cup ya UEFA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269