Nimekamilisha vikao vya usalama
mitandao vilivyofanyikia jijini Nairobi kufuatia mualiko maalum
nilioupata. Katika vikao hivyo niliwasilisha mada mbili (ya kwanza ikiwa
ni namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao na mada ya pili ikiwa ni
namna ya uchunguzi wa makosa ya digitali kitaalam) katika mada hizo
mbili ambazo zilipokelewa vizuri na kupelekea mijadala ya kipekee kuna
mengi nikajifunza kutoka kwa washiriki. Aidha, nilishiriki mijadala
duara iliyojikita katika changamototo mbali mbali za uhalifu mitandao na
kuiangazia sharia mtandao ya nchi ya Kenya.
Kenya ni miongoni mwa nchi tatu
barani afrika ambazo zimeorodheshwa kua na uhalifu mkubwa sana wa
kimtandao nyingine ni Nigeria pamoja na Afrika ya kusini. Tukijadili
takwimu za kutisha duniani kote, tulishuka na kuangazia bara la Afrika
na baadae Afrika mashariki na hatimae kujikita na twakwimu za Nchi ya
Kenya.
Kwa upande wa Kenya kwa mujibu
wa takwimu zilizo wasilishwa katika mkutano, hadi kufikia Mwezi wa saba
mwaka huu (2015) kuna simu 34.8 Milioni huku watumiaji wakiwa ni 26.0
Milioni. Aidha, matumizi ya intaneti ni 29.1 milioni ambayo ni sawa na
65% “penetration”. Takwimu hizo zinasindikizwa na upotevu wa dola za
kimarekani 20 milioni ($20 Mil) kila mwaka kutokana na uhalifu mtandao.
Palizungumzwa matukio ya
kudukuliwa kwa tovuti Nchini humo ambapo, tovuti za serikali 103
ziliathiriwa mwaka 2013, na 3 kwa mwaka wa 2014 huku twitter ya serikali
mwaka jana (2014) ikiwa ni miongoni mwa zilizo dukuliwa na kutumiwa
vibaya. Nilihoji tofauti kubwa ya udukuzi wa tovuti na kujulishwa baada
ya tukio la aina yake la mwaka 2013 serikali iliamua kuzifunga tuvuti
zake nyingi hasa zile zilizo onekana hazina umuhimu sana kua hewani kitu
ambacho kilichangia kupunguza namba kubwa ya udukuzi kwa mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269