Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (wa kwanza kulia)
akisaini hati ya makubaliano katika hafla ya utiaji saini wa mikataba 2
ya sekta za maji, afya na maliasili Alhamisi Agosti 13, 2015 Jijini Dar
Es Salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe.
Egon Kochanke.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akiongea na baadhi ya
viongozi wa Wizara hiyo, ujumbe wa ulioandamana na Balozi wa Ujerumani
pamoja na waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini wa mikataba 2
ya sekta za maji, afya na maliasili
Balozi
wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke akiongea na baadhi ya
viongozi wa Wizara ya Fedha, wajumbe kutoka Ujerumani pamoja na
waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za
maji, afya na maliasili
Viongozi
kutoka Wizara ya Fedha, wajumbe kutoka Ujerumani pamoja na waandishi wa
habari waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za
maji, afya na maliasili Alhamisi Agosti 13, 2015 Jijini Dar Es Salaam
.
Na Jenikisa Ndile-MAELEZO
Serikali
ya Tanzania na Ujerumani zimetiliana saini mikataba miwili ya misaada
yenye thamani ya jumla ya Euro milioni 17 ambazo ni sawa na Tsh. Bilioni
39.1 kusaidia sekta ya afya, maji na maliasili.
Makubaliano
hayo yamesainiwa jijini Dar es salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke ili kuleta mafanikio
na maendeleo katika.
Aidha,
Dkt. Likwelile amemhakikishia Balozi Kochanke na ujumbe wake kuwa
msaada walioipa Serikali utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta
ufanisi na kuongeza nafasi za ajira na hatimaye kuchangia katika
kuboresha uchumi nchini.
Kwa
upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke amesema
kuwa serikali ya Ujerumani itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa
kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Zaidi
ya hayo, serikali hizo mbili zimesaini mkataba wenye thamani ya Euro
milioni 10 ambazo ni sawa na Tsh bilioni 23 kuisaidia usimamizi wa
hifadhi ya Taifa ya ya wanyama mwitu ya Selous
Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269