Mgeni
Rasmi ambaye ni Afisa Vijana Halmashauri jiji la Mbeya Onah Temu
akitoa hotuba katika siku ya Vijana Duniani ambayo kwa Mkoa wa Mbeya
ilifanyikia Ukumbi wa Chuo kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya.
Maandamano kuelekea katika Ukumbi ambapo vijana wanakutana kwa ajili ya Sherehe yao
Mratibu wa Mradi wa Restless Fadhiri Mtanga akitoa mada kuhusu Maendeleo ya Vijana
Wakili Stephen John akiwashauri vijana kuto tumika na wanasiasa
Muwezeshaji wa Sherehe hiyo ya Vijana Mwadawa Mbando akiendelea kutoa utaratibu
Vijana wakisikiliza kwa makini watoa mada kaika sherehe hiyo iliyofanyika ukumbi wa Mzumbe Mbeya
Mmoja wa vijana kulia akipokea zawadi baada ya kupokea zawadi
William Otuku akitoa Maada kuhusu afya ya Uzazi kwa vijana
Picha ya pamoja
KATIKA
maadhimisho ya siku ya Vijana duniani yaliyofanyika Kimkoa katika
ukumbi wa Chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya, Vijana wamekumbushwa
kuhusiana na afya ya uzazi kwa vijana pamoja na maendeleo yao.
Aidha
katika kongamano hilo ambalo liliandaliwa na mashirika binafsi ya
Restless Developmentna Young & alive initiative ambalo lilihudhuriwa
na Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu na shule za Sekondari za Jiji la Mbeya.
Akizungumza
katika kongamano hilo mwakilishi wa Shirika la Young & Alive
Initiative, William Otuku, alisema lengo la maadhimisho hayo ni
kuwakumbusha vijana kuhusiana na maswala yanayohusu afya ya uzazi kwa
vijana ili waweze kuwa na uwezo wa kushiriki shughuli za maendeleo
wakiwa salama.
Aliongeza kuwa kauli mbiu ya siku hiyo ni kuhakikisha vijana wanashirikishwa na kuhusishwa katika
kupanga maamuzi mbali mbali hivyo hayo yote yanaweza kutimia endapo
wataelimishwa kuhusiana na afya ya Uzazi ili waliomashuleni waendelee
kufanya vizuri na kusaidia kutoa elimu kwa ambao hawako mashuleni.
“Vijana tunawapa elimuya afya ya
uzazi ili waweze kuwa imara katika kushiriki shughuli za maendeleo za
kijamii pamoja na kuwaepusha na vitendo ambavyo vitaweza kuwaondolea
katika hatari ya kupata magonjwa yanayoweza kuepukika” alisema Otuku.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Shirika
la Restless Development,Fadhili Mtanga, alisema lengo la kongamano hilo
ni kujadiliana kwa pamoja kuhusiana na changamoto ambazo zinawakabili
vijana pamoja na kubadilishana mawazo juu ya kuweza kutatua na
kukabiliana na vikwazo vya maendeleo kwa vijana.
Alisema
lengo la kuwahusisha wanafunzi ni kutokana na kuwa na kundi kubwa la
vijana wanaoanzia umri kati ya miaka 15 hadi 35 ambao ni kundi kubwa
katika jamii hivyo ni rahisi kwao kupeleka mabadiliko kwa wananchi
wengine ambao hawakubahatika kuhudhuria kongamano hilo.
“Sisi
tumewalenga zaidi vijana ambao ni wanafunzi kwa sababu tunaamini
wanakubalika kaika jamii na nirahisi kwao kutoa elimu ambayo iaweza
kuwafikia wahusika kwa haraka zaidi” alisema Mtanga.
Naye
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo, Afisa Vijana wa Jiji la Mbeya, Ona
Temu kutoka Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Jiji la Mbeya, alipongeza kwa
wadau kujitokeza na kuandaa kongamano hilo kwa kutambua mchango wa
vijana katika jamii.
Alisema
vijana wanapaswa kuutumia vizuri umri kati ya miaka 18 hadi 40 kwa
kujenga na kutafuta uchumi ili kipindi cha miaka 40 hadi 60 anabaki kuwa
msimamizi wa shughuli ambazo alizifanyia kazi kipindi cha ujana wake.
Aliongeza
kuwa kipindi cha umri wa zaidi ya miaka 60 ni muda wa kufaidi matunda
na kupumzika kwani utakuwa tayari umeshafanya kazi ya kutafuta na
kuzisimamia vizuri kwa malengo makubwa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269