Bi. Samia Othuman Suluhu akipokewa na baadhi ya viongozi na makada wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
BAADHI
ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamelazimika
kuuzuia msafara wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais leo alipokuwa
njiani akitokea Wilaya ya Same kuelekea Wilayani Mwanga mkoani
Kilimanjaro huku wakimuomba awasalimu na kuzungumza nao, kabla ya
kuendelea na safari yake.(P.T)
Bi.
Samia Suluhu alilazimika kuusimamisha msafara wake baada ya wananchi
hao kusogea zaidi barabarani wakati akipita huku wakinyoosha mikono ya
kumuomba asimame ili azungumze nao eneo la kilometa chache kabla ya
kuingia njia panda. Wananchi hao wengi wakiwa wakinamama walimsimamisha
kwa kuingia pembezoni mwa barabara alipokuwa akipita na hivyo kulazimika
kusimama kwa dakika chache na kuzungumza nao.
Akizungumza
aliwaambia amefarijika na kuwaona na mapenzi makubwa na chama chao
hivyo kuwaeleza kuwa yeye ni mwanamke pia na anajua kwa karibu kero
ambazo wanakabiliana nazo akinamama sehemu mbalimbali na kuahidi endapo
watapata ridhaa pamoja na Dk. John Magufuli atahakikisha anasimamia
vizuri utaratibu wa kuwawezesha akinamama kupitia vikundi vya kijamii
ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na familia zao.
Alisema
yeye ni mwanamke mzazi anatambua shida wanazokumbana nazo akinamama
hasa kwenye wodi za wazazi hivyo akifanikiwa kuingia madarakani
atahakikisha anasimamia ipasavyo ilani ya chama ambayo imeeleza vizuri
juu ya uboreshaji huduma za afya ikiwemo wodi za akinamama na hali ya
upatikanaji madawa.
"...Matatizo ya wanawake nayafahamu vizuri wala sisimuliwi maana na
mimi ni mzazi nimeingia wodi ya wazazi mkitupa ridhaa na mwenzangu
(mgombea urais, Dk. Magufuli) nitahakikisha nayasimamia haya vizuri,"
alisema Bi. Suluhu akizungumza muda mfupi na wananchi waliomzuia
barabarani wakiomba awasalimu.
Alisema
kero ya maji imekuwa inawatesa akinamama kwa kutumia muda mwingi
kutafuta maji na kushindwa kuzalisha uchumi wa familia ipasavyo, hivyo
Serikali ya CCM imeanza mradi wa kutoa maji katika Bwawa la Nyumba ya
Mungu na kuyaingiza katika vijiji vyenye shida ya maji.
Aidha
akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara Mwanga ameisikia kero ya
uhaba wa mabweni kwa wanafunzi wa kike suala ambalo linachangia kwa
kiasi kikubwa mabinti hao kutiwa mimba na kukatisha masomo eneo hilo na
kudai suala hilo lipo katika ilani ya CCM mwaka huu na litashughulikiwa
vizuri endapo watapewa ridhaa na wananchi, ikiwa ni pamoja na suala zima
la kupambana na kuongeza fursa za vijana ili kukabiliana na uhaba wa
ajira.
Alisema
Serikali iliyopita imejitahidi kuongeza huduma za umeme katika vijiji
ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi lakini katika awamu hii CCM ikipewa
ridhaa itahakikisha vijiji vilivyobaki kwa baadhi ya maeneo vinawekewa
umeme. Alisema anawapa akinamama kazi kuhakikisha Dk. Magufuli na
wagombea wa CCM eneo hilo wanashinda kwa asilimia 80 kwani wao ndio
wenye ushawishi mkubwa katika familia.
Vivyo
hivyo kuwataka madiwani wanaogombea kuhakikisha mgombea uraisi na
wengine wanapata kura za kutosha ili kushinda uchaguzi. Kwa upande wake
Asumta Mshana aliyekuwa mbunge wa CCM na uchaguzi huu aligombea na kura
hazikutosha alisema anawashangaa wanachama ambao waligombea ndani ya
Chama Cha Mapinduzi na waliposhindwa wakaamua kuondoka ndani ya chama
hicho. Alihoji kwani walipokuwa wakiomba nafasi hizo hawakutambua kuna
kushindwa na kushinda? Aliwafananisha wanaofanya hivyo ni sawa na
akinababa wanaoamua kukimbia familia zao jambo ambalo ni aibu.
"Nawashauri
wababi ndani ya chama na kukijenga chama ili kiweze kufanya vizuri,
kama kura hazikutosha safari hii usikimbie chama kwani mlikuwa hamjui
kuna kushinda na kushindwa unapoomba uongozi," alisema. Naye Mwenyekiti
wa CCM, Mkoa Idd Juma Mohamed alimshukuru Bi. Samia kwa kuamua kuanza
kampeni katika mkoa wake na kumuhakikishia watahimiza wapiga kura kwani
Kilimanjaro bado ni ngome ya CCm na watahakikisha wanatwaa majimbo yote,
viti vya udiwani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269