Wanachama wa muungano unaoongozwa na
Marekani kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State wameitaka Urusi
kusitisha mashambulio kutoka angani wakisema yanadhuru makundi
yanayompinga Bashar al-Assad pamoja na raia.
Kupitia taarifa ya
pamoja iliyotolewa Ijumaa, Marekani, Uingereza, Uturuki na mataifa
mengine ya muungano huo yalisema mashambulio ya Urusi yatazidisha kuwepo
kwa makundi yenye itikadi kali
Urusi, ambayo kwa mujibu wa mashahidi ilianzisha tena mashambulio Ijumaa, inasema inalenga IS.
Afisa mkuu wa Urusi anasema mashambulio hayo huenda yakaendelea kwa miezi mitatu hadi mine.
Alexei
Pushkov, mkuu wa kamati ya mashauri ya kigeni katika bunge la Urusi,
aliongeza kuwa Marekani ilikuwa tu “ikijifanya” kuangushia mabomu IS na
akaahidi kwamba kampeni ya Urusi itafanikiwa zaidi.
Jeshi la angani la Urusi lilianza kushambulia maeneo ya Syria Jumatano.
Jeshi
la Syria linasema Urusi ilitekeleza mashambulio 18 tangu Alhamisi
jioni. Inasema baadhi ya mashambulio hayo yalitekelezwa Hama na Idlib,
mikoa ambayo haina wapiganaji wa Islamic State kwa wingi.
Wizara
ya Ulinzi ya Urusi ilisema ndege zake za kijeshi zilishambulia ngome ya
IS eneo la Raqqa Alhamisi. Wanaharakati wanasema wapiganaji kadha wa IS
waliuawa huko.
Mashambulio hayo ya ndege Syria ndiyo operesheni ya
kwanza ya kijeshi wa Urusi nje ya eneo la uliokuwa Muungano wa Usovieti
tangu kumalizika kwa Vita Baridi.
Onyo la mataifa ya muungano huo
unaoongozwa na Marekani limetolewa huku viongozi wa Ufaransa na Urusi
wakitarajiwa kukutana baadaye Paris.
Mkutano huo uliitishwa kujadili juhudi za kutafuta amani Ukraine, lakini sasa hilo huenda likagubikwa kwa Syria.
Upinzani
nchini Syria umedai makundi ya waasi yanaompinga Rais wa Syria Bashar
al-Assad, ambaye ni mshirika wa Urusi, nadiyo yanayoumizwa Zaidi na
mashambulio ya Urusi.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi Sergei
Lavrov, akiongea katika makao makuu ya UN New York, alisema Urusi
itashambulia pia makundi mengine ya kigaidi likiwemo al-Nusra Front,
lenye ushirika na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda.
"Hatuungi mkono kundi lolote. Tunapigana na ugaidi,” alisema.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269