Theresia Mmasy Afisa masoko
kutoka kampuni ya ALAF iliyodhamini tuzo hizo akizungumza na waandishi
wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati akielezea
tuzo za shindanio la kuandika riwaya za kiswahili zilizofanyika jijini
Nairobi Nchini Kenya hivi karibuni na watanzania kuibuka washindi katika
vipengere mbalimbali.
Enock Maregesi mshindi
wa uandishi wa riwaya ya Kiswahili ya Kolonia Santita riwaya iliyoshinda
katika mashindano ya uandishi wa riwaya za Kiswahili yaliyofanyika
jijini Nairobi Nchini Kenya akipokea tuzo yake kutoka kwa Piyush Kanti
Nath Meneja Huduma na Masoko wa ALAF kampuni iliyodhamini tuzo hizo ,
Katikati ni Vikrant Srvanstava Meneja Mauzo ALAF.
…………………………………………………………………………………………………………
KWA mara ya kwanza Lugha ya Kiswahili imeingia katika
rekodi ya dunia kwa watanzania wanne kuchomoza katika tuzo ya waandishi
ya Fasihi Afrika.
Akizungumza na wa
andishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mshiriki wa
Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian
Mtembei amesema lugha ya Kiswahili ya kujivunia kutokana na watanzania
wenye lugha yao kuwa washindi.
Washindi wa tuzo hizo ni Enock
Maregesi ambaye aliandika Kolonia Santita,Chiristophee Bubebah, Anna
Manyaza aliandika Penzi la Damu, Mohamed Ghassani aliandika N’na Kwetu.
Walioshiriki katika tuzo hiyo
walikuwa 65 na kuweza kuibuka watu wanne ambao ni washindi wakitokea
nchini na sherehe hizo zilifanyika Nchini Kenya.
Amesema kwa lugha ya kifaransa
na Kiingereza zimekuwa zikijitokeza kila mwaka kwa watu kuandika riwaya
na mashairi lakini Kiswahili imekuwa ikisahaulika hivyo na kufanya Chuo
Cornell Nchini Marekani iliamua kufanya hivyo kuwa watu kuandika Riwaya
na Mashairi.
Katika tuzo hizo Kampuni ya
watengenezaji wa Mabati ya ALAF ilidhamini tuzo hizo na kutaka watu
wajitokeze katika kuinua lugha ya Kiswahili duniani.
Afisa Masoko wa
Alaf,Theresia Mmasy amesema kazi wataendelea kushirikiana na watanzania
katika kukuza Kiswahili katika kudhamini tuzo hizo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269