Aliyekuwa
mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi Mboni Mhita kushoto akimkabidhi mwenge
aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Bi Angelina Mabula ,wote Hawa kwa
sasa ni wabunge wa majimbo huku Mabula ni Naibu Waziri wa Nyumba , Ardhi
na makazi
Mwenyekiti wa Faraja Saccos Bi Marcelina Mkini akipongezwa na kiongozi wa mbio za mwenge kulia ni Bi Mboni akishuhudia
Halmashauri
ya Wilaya ya Mufindi ya Mkoani Iringa imeibuka mshindi wa kwanza kimkoa
na kushika nafasi za juu kikanda na kitaifa, kati ya Halmashauri tano
za Mkoa wa Iringa, baada ya kufanya vizuri zaidi wakati wa mbio za
mwenge wa uhuru ulipokimbishwa Mkoani Iringa mnamo mwezi Juni mwaka huu.
Taarifa
ya kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi imevitaja baadhi ya vigezo kati ya vigezo 10
vilivyoshindanishwa, kuwa ni pamoja na miradi yenye maslahi kwa umma
iliyozinduliwa wakati wa mbio za mwenge wa uhuru, uimarishaji wa vikundi
vya uzalishaji mali kwa wanawake na vijana.
Vigezo
vingine vinavyozingatiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya Malaria, dawa
za kulevya, michango ya Mwenge wa uhuru sanjari na mapokezi ya mwenge
wenyewe ulipowasili wilayani Mufindi
Akizunguzia
ushindi huo, Mkuuwa wilaya ya Mufindi JOWIKA KASUNGA amewashukuru
wakazi wa Mufindi na wadau wa maendeleo kwa michango yao pamoja na
kushiriki mbio za Mwenge wa uhuru na akatoa rai ya kundelea kuuenzi
mwenge wa uhuru kama alama na utambulisho wa taifa.
Aidha,
taarifa hiyo imezitaja nafasi ilizoshika kuwa ni ushindi wa kwanza
kimkoa, ushindi wa 05kwa kanda ya kiuchumi yenye zaidi Halmashauri 36
pamoja na nafasi ya 22 kitaifa ikijumuisha zaidi ya Halmashauri 140.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269