Afisa Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani)jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwandishi wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi na Mwandishi wa Ushairi la Kifaurongo, Christopher Budebah.
Mkuu wa Idara ya Fasihi ya Mawasiliano na Uchapishaji (TATAKI) WA wa chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwa na baadhi ya viongozi ya ALAF Limited.
Mshiriki wa Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian Mtembei akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
KWA mara ya kwanza Lugha ya Kiswahili imeingia katika rekodi ya dunia kwa watanzania wanne kuchomoza katika tuzo ya waandishi ya Fasihi Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mshiriki wa Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian Mtembei amesema lugha ya Kiswahili ya kujivunia kutokana na watanzania wenye lugha yao kuwa washindi.
Washindi
wa tuzo hizo ni Enock Maregesi ambaye aliandika Kolonia
Santita,Chiristophee Bubebah, Anna Manyaza aliandika Penzi la Damu,
Mohamed Ghassani aliandika N’na Kwetu.
Walioshiriki
katika tuzo hiyo walikuwa 65 na kuweza kuibuka watu wanne ambao ni
washindi wakitokea nchini na sherehe hizo zilifanyika Nchini Kenya.
Amesema
kwa lugha ya kifaransa na Kiingereza zimekuwa zikijitokeza kila mwaka
kwa watu kuandika riwaya na mashairi lakini Kiswahili imekuwa
ikisahaulika hivyo na kufanya Chuo Cornell Nchini Marekani iliamua
kufanya hivyo kuwa watu kuandika Riwaya na Mashairi.
Katika
tuzo hizo Kampuni ya watengenezaji wa Mabati ya Alaf ilizamini tuzo hizo
na kutaka watu wajitokeze katika kuinua lugha ya Kiswahili duniani.
Afisa
Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy amesema kazi wataendelea kushirikiana na
watanzania katika kukuza Kiswahili katika kudhamini tuzo hizo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269