DC. Paul Makonda |
Mnamo
tarehe 23 wilaya yangu iliamua kufanya upimaji wa bure wa magonjwa ya
moyo, upimaji ambao niliamini ungebeba faida kubwa nne: moja, kujenga
utamaduni wa kupima afya mara kwa mara miongoni mwa wananchi, pili
kubaini watu ambao tayari wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo, tatu
kuchukua hatua za awali za kuwasaidia wale ambao tayari
wameshashambuliwa na magonjwa hayo na mwisho kutoa elimu juu ya namna ya
kujikinga dhidi ya magonjwa yote ya moyo.
Ugonjwa
wa moyo ni ugonjwa unaoweza kuzalisha magonjwa mengi sana na kama
hujafanya vipimo sahihi ni rahisi kushughulika na matokeo ya ugonjwa
huku ukiacha chanzo kikizaa magonjwa mengine. Mathalani, unaweza
kujikuta unahangaika na kuvimba kwa miguu au kuhangaika na macho ama
figo aukisukari na hata kupoteza nguvu za kiume ukifikiri ndio tatizo
kumbe tatizo la msingi ni moyo.
Kimsingi
ni kwasababu hizo nilizozianisha nilichukua hatua ya kukiomba taasisi
ya moyo ya Jakaya Kikwete kinachosimamiwa na Profesa Janabikinisaidie
kutoa huduma hiyo bure ndani ya wilaya yangu.
Napenda
kuchukua nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza sana madaktari kutoka
taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na mwananyamala kwa kuitikia
wito na kushiriki kikamilifu kulifanya zoezi hilo. zoezi ambalo lilikuwa
kubwa na zito kwani kwa makadirio ya awali tulitegemea kupata watu
wasiozidi 2000 ila badala yake walijitokeza wananchi zaidi ya 7000 ila
kutokana na umahiri wa madaktari hao tuliweza kuhudumia zaidi ya
wananchi 5900 ingawa tulilazimika kulifanya zoezi hilo kwa siku ya pili
yake ambayo ilikuwa ni tarehe 24.
Na
kwa watu wengine zaidi ya 1200 waliokuwa wamebaki, zoezi lao
tulilipanga na kulifanya tarehe 30 ya mwezi huu huu wa kwanza. Ukweli ni
kwamba, mambo mengi yalijitokeza kwa siku hizi tatu za upimaji; wapo
waliolazimika kukimbizwa kwa ambulance kuelekea hospitali za
mwananyamala na muhimbili, wapo waliolazimika kupewa appointments za
kuwaona madaktari, wapo waliopewa ushauri wa matumizi ya dawa na wengine
kubadilishiwa dawa sambamba na maelekezo ya utumiaji wa chakula na
ufanyaji wa mazoeziili kupunguza uzito.
Nichukue
tu fursa hii kuwapongeza wanakinondoni kwa kuitikia wito na kuniamini
mkuu wao wa wilaya na serikali yangu kwa ujumla kwamba tuna nia njema na
tunawapenda wananchi wetu kwa kuwahakikishia afya zao zinastawi na
kuendelea kuwa bora siku zote.
Kutokama
na maelezo niliyoyatoa hapo juu sambamba na sababu zilizonisukuma
kufanya zoezi hilo na kutokana na muitikio mkubwa wa wananchi bila
kusahau matokeo ya vipimo vilivyofanyika na kupata majibu ya kwamba watu
wengi wanahitaji matibabu, kubadilishiwa dawa, maelekezo ya matumizi
sahihi ya vyakula pamoja na mazoezi nimefanya uamuzi wa kulifanya zoezi
hili la kudumu na tayari nimeshafanya mazungumzo na hospitali kubwa na
nimetafuta njia na utaratibu bora zaidi wa kulifanya zoezi hili kuwa ni
zoezi la kudumu.
Sasa
basi, natamka rasmi kuwa serikali ya wilaya ya kinondoni inaanza
utaratibu wa kupima bure mara tatu kwa mwaka, utaratibu ambao utaanza
katikati ya mwezi wa nne. Zoezi hili litafanyika kwa kupima zaidi ya
magonjwa kumi ikiwemo yafuatayo: moyo, kisukari, kansa, macho, figo,
meno, kifua kikuu (TB), typhoid, magonjwa ya ngozi, presha, animonia,
kansa ya kizazi, kansa ya matiti, mabusha na matende.
Kama nilivyosema hapo awali ya kwamba, nimeshafanya mazungumzo na hospitali kubwa na kila hospitali itatoa vitengo viwili au vitatu na utaratibu utakuwa hivi. Kwa mfano, utakuta banda limeandikwa Jakaya Kikwete Cardiac Institute ndani ya banda hilo utakuta madaktari waliobobea kwenye upande wa moyo na upimaji wa presha kwahiyo mtu anayetaka kupima moyo ama presha atakwenda moja kwa moja kwenye banda husika.
Kama nilivyosema hapo awali ya kwamba, nimeshafanya mazungumzo na hospitali kubwa na kila hospitali itatoa vitengo viwili au vitatu na utaratibu utakuwa hivi. Kwa mfano, utakuta banda limeandikwa Jakaya Kikwete Cardiac Institute ndani ya banda hilo utakuta madaktari waliobobea kwenye upande wa moyo na upimaji wa presha kwahiyo mtu anayetaka kupima moyo ama presha atakwenda moja kwa moja kwenye banda husika.
Ama
unaingia kwenye banda limeandikwa Ocean Road hospital kwahiyo yeyote
anayetaka kupima kansa ataingia humo…hivyo hivyo kwa magonjwa mengine
yote: kutakuwa na mabanda tofauti yaliyoandikwa ni hospitali gani na
wanapima magonjwa gani, lengo ikiwa ni kumpa urahisi mpimaji
atakayejitokeza.
Mwisho
ila si kwa umuhimu niwashukuru sana wananchi wote wa wilaya nyingine na
wale waliotoka mikoa mbalimbali ikiwemo Tanga, Pwani, Morogoro, Lindi
na Dodomakwa imani yao kubwa juu ya tukio hili iliyowafanya kutoka mbali
na kujisogeza mpaka viwanja vya leaders wakiwa na imani ya kupatiwa
huduma hata kama zoezi hili lilikuwa limewalenga wakazi wa wilaya ya
Kinondoni.
Sambamba
na kuwashukuru wananchi niwashukuru pia waandishi wa habari ambao
wamekuwa mstari mbele kulitangaza tukio na kuhakikisha wananchi wanapata
taarifa kwa wakati.
Imetolewa na:- Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda
Imetolewa na:- Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269