Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Nnauye akifungua Mwaka Mpya Kichina wa 2016
unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo
mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto
ni mshereheshaji aliyejitambulisha kwa jina la “Sharobaro”.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri
Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim Ahmed
Salim (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kichina wa 2016
unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo
mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kulia) akifuatilia michezo mbalimbali
wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016
unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo
mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto
ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini
Tanzania Gao Wei.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Nnauye (katikati) akifuatilia michezo mbalimbali
wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016
unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo
mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia
ni Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Salim Ahmed Salim na kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka
Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akisalimiana na Waziri Mkuu
Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda
(kulia) alipowasili viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere”
Baadhi ya wageni waliohudhuria
hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016
Baadhi ya raia wa Kichina
wakiendelea na kujipamba kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa Mwaka
Mpya Kichina wa 2016
Baadhi ya michezo iliyooneshwa
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana
kama mwaka wa “Ngedere”
Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akichanganya tiketi za
bahatinasibu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016
unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere”
Vimulimuli vy fataki zilizowashwa
kuashiria kuzinduliwa kwa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama
mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.(Picha na Eleuteri
Mangi-MAELEZO)
………………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Jumuiya ya Wachina wanaoishi
nchini wamezindua na kuukaribisha kwa shamrashamra mwaka Mpya wa 2016
unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo
mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Akizindua shamrashamra hizo,
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alisema kuwa
Wachina na Watanzania ni ndugu ambao uhusiano wao ni wa kudumishwa
milele na milele.
“Uhusiano wa Tanzania na China ni
wa kihistoria ambao ni wa muda mrefu katika mambo mbalimbali ikiwamo
kijamii, kiuchumi, kisiasa, kielimu na kiutamaduni Utamaduni na
kimawasiliano kati ya nchi hizi mbili” alisema Waziri Nape.
Kihistoria, uhusiano wa China na
Tanzania ni wa kidugu na kirafiki wakati wote iwe wa dhiki au faraja
katika maisha ya kila siku kati ya Watanzania na Wachina.
Ni wakati muafaka kuongeza
jitihada za kuimarisha uhusiano na ushirikiano wan chi hizo mbili ili
kuwaenzi waasisi wa ushirikiano huo ambao ni Rais Mwalimu Julius Nyerere
na Mao Tse Tung.
Kwa upande wake Mshauri wa Mambo
ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei alisema
kuwa wanajisikia faraja wakati wote wanapofanya kazi na Watanzania kwa
kuwa wanamengi ya kujivunia katika historia ya nchi hizo.
Aidha, shamrashamra za mwaka mpya
wa Kichina zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Mawaziri Wakuu
Wastaafu Salum Ahmed Salum, Mizengo Pinda, viongozi mbalimbali na
wenyeji wa sherehe hizo ambao ni raia wa Kichina wanaoishi nchini
wakiongozwa na viongozi kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania.
Mwaka huu unajulikana kama
“Ngedere” wakati mwaka 2015 ulijuklikana kama “Kondoo” ambapo
maadhimisho ya Mwaka Mpya wa “Ngedere” yalipambwa na michezo mblimbali
ikiwemo bahatinasibu, sarakasi, nyimbo, muziki wa ala, mazingaombwe na
ngoma.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269