Meza kuu kwenye uzinduzi wa kambi
ya upimaji afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano
iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania
(Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana
jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mratibu wa kambi hiyo ya upimaji
kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk.Ali Mzige, Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii
ya watu kutoka India, Bengali waliopo Tanzania (Bango Sangho), Kunal
Banerjee, Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kibugumo, Mzamilo Ally, Mgeni
rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Jimbo
la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Umoja wa Watu kutoka Bengali, India
wanaoishi nchini (Bango Sangho) umetoa msaada wa kompyuta, printa, tanki
la maji la lita 5000, umeme, madarasa saba yaliyofanyiwa ukarabati,
madaftari na kalamu katika Shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni
ulio na thamani ya shilingi Milioni 20 pamoja na huduma ya kupima afya
kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano.
Akizungumzia msaada huo, Mwenyekiti
wa Bango Sangho, Kunal Banerjee alisema wameamua kutoa msaada huo kwa
shule ya Msingi Kibugumo na huduma ya kupima bure kwa kutambua umuhimu
wa afya na elimu bora kwa maendeleo ya sasa na baadae kwa taifa.
Alisema wamekuwa wakitoa misaada
katika shule hiyo kwa mwaka wa tatu mfululizo na mwaka huu waliamua
kuwaletea tena na huduma ya upimaji afya bure kwa watoto walio na umri
chini ya miaka mitano ili wazazi wapate fursa ya kutambua hali ya afya
za watoto wao lakini pia kuwajengea utaratibu wa kuwapeleka watoto wao
katika vituo vya afya ili kujua hali zao za kiafya,
“Sisi tunapenda kuona hali nzuri ya
elimu na tumeshasaidia kwa muda shule hii tumeshatoa madawati 100 na
tulijenga madarasa mawili na leo tumeleta msaada mwingine na pia awamu
hii tena tumeleta huduma ya afya ili watoto wapimwe afya zao,” alisema
Banerjee.
Mwenyekiti wa Bango Sangho,
Kunal Banerjee akisoma risala ya Umoja huo mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa
Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk.
Faustine Ndungulile.
Nae mgeni rasmi katika halfa hiyo ya
kupokea msaada kutoka Bango Sangho, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi.
Sophia Mjema aliwashukuru Bango Sangho kwa msaada huo ambao wameotoa
katika shule hiyo na huduma ya kupima afya kwa watoto walio na umri
chini ya miaka mitano na kuwaomba kama ikiwezekana wawapelekee huduma
hiyo ya kupima afya kila baada ya miezi
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269