WATU
wanaosadikiwa kuwa majambazi, wamenusurika kifo baada
ya wananchi wenye hasira, kuyaweka “mtu kati” neo la Kariakoo jijini Dar es
Salaam mida hii.
Msomaji
wa K-VIS Blog amerusha picha zinazoonyesha majambazi mawili yakiwa hoi bin
taaban kwenye eneo la tukio baada ya polisi wenye silaha kuwahi kwenye eneo
hilo na kuyaokoa yakiwa tayari yanavuja damu.
Kama
ilivyo kawaida, mamia kwa maelefu ya watu wanaotafuta mahitaji eneo hilo la
Kariakoo waliyazingira majambazi hayo baada ya jaribio lao la kupora fedha
kushindwa.
Taarifa
kamili itawajia kadrizitakavyotufikia
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269