WAKATI
wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, (CAF Champions league), Yanga ikitolewa na
El-Ahly National ya Misri kwa jumla ya mabao 3-2 usiku wa kuamkia leo Aprili
21, 2016, polisi mjini Alexandria, walilazimika kurusha mabomu ya machozi
kusambaza washabiki wa timu hiyo kongwe ya waarabu.
Polisi
walichukua uamuzi huo kuwatawanya maelfu ay washabiki wa El-Ahli waliotaka
kuingia kwenye uwanja wa Borg El-Arab mjini Alexandria, ambapo Yanga ilikuwa
ikimenyana na El-Ahli kwenye mchezo wa marudiano raundi ya 16 ya michuano hiyo
ambapo katika pambano hilo, Yanga ilifungwa mabao 2-1 na hivyo kutolewa kwenye
michuano hiyo kwa jumla ya mabao 3-2 ikizingatiwa kwenye mchezo wa awali
uliochezwa jijini Dar es Salaam wiki moja iliyopita, timu hizo zilitoka are ya
bao 1-1 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
ATaarifa
ya polisi mjini Alexandria ilisema “Tulijaribu kuwashawishi waondoke, lakini
walipinga na kujaribu kuingia uwanjani kwa nguvu ambapo polisi wa kutuliza
ghasia walilazimika kufyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanya” taarifa hiyo
ilisema.
Watu 29 walipoteza fahamu kwenye ghasia hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269