Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya
kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.
NA; BMG
Tukio hilo
limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo
ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia
mnarani hadi majira ya saa sita mchana
Mashuhuda wa tukio
hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda
kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao
amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na
matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia
Akizungumza kwa
niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja
wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni yenye
minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari
inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.
Baadhi ya
mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana
huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa,
ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa
ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati
ya mnara huo.
Baada ya kijana
huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na
kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa
ajili ya huduma ya kwanza
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269