Msanii
wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Neyo amewasili jijini Mwanza jioni
hii akitokea Dar es Salaam na kupokelewa na umati mkubwa wa wakazi wa
jiji hilo kama Mfalme katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.
Msanii
wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akiondoka katika hoteli ya
Hyatt Regency-The Kiliamanjaro kueelekea katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa safari ya jiji Mwanza kutumbuiza
kwenye Jembeka Festival 2016 .
Meneja
Masoko wa CFAO Motors Group, Attu Mynah ambao wamedhamini usafiri
uliotumika kumwendesha msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo
gari aina Mercedes Benz GLE 350 D ya mwaka 2016 katika picha ya
kumbukumbu na Msanii huyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere.
Msanii
wa kimataifa Neyo aki-show love na walinzi maalum kabla ya kuelekea
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa
safari ya Mwanza.
Msanii
wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akielekea kwenye gari maalum
aina ya Mercedes Benz GLE 350 D ya 2016 lilitolewa na kampuni ya CFAO
Motors Group.
Msanii
wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili uwanja wa
ndege wa Mwalimu JK Nyerere akiwa amezungukwa na walinzi maalum
alipokuwa akielekea jijini Mwanza.
Msanii
wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili kwenye uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na mlinzi wake
wakielekea jijini Mwanza leo jioni.
Balozi
wa Umoja wa Mataifa mtoto mwanabadiliko wa mazingira, Getrude Clement
akimvisha shuka la kimasai Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,
Neyo baada ya kuwasili jijini Mwanza leo jioni.
Msanii
wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo aki-'show love' na Balozi wa
Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Umoja wa Mataifa, Getrude Clement
aliyefika uwanjani hapo kumlaki na kumvisha shuka la Kimasai.
Msanii
wa kikundi cha ngoma cha Bujora Cultural Troupe cha jijini Mwanza
akimshikisha nyoka aina chatu msanii wa kimataifa kutoka nchini
Marekani, Neyo alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii.
Waandishi wa habari wa jijini Mwanza wakiwemo wa JEMBE FM wakifanya mahojiano na msanii Neyo alipowasili jijini Mwanza.
Wakazi
wa jijini Mwanza wakisalimana na msanii Neyo kwa shangwe na furaha
waliofika kumlaki katika uwanja wandege wa jijini Mwanza.
Msafara wa msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo ukielekea hotelini baada ya kuwasili jijini Mwanza.
Msanii
Neyo alipowasili kwenye hoteli ya Malaika Resorts ya jijini Mwanza
akiwapungia wafanyakazi pamoja na wateja katika hoteli hiyo.
Mwanasheria
wa Jembe Media Group, Justine Ndege katika picha ya pamoja na Msanii wa
kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo katika hoteli ya Malaika Resort.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana
mawazo na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo anayetarajiwa
kutumbuiza kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla
(t-shirt ya blue) na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo
wakijianda kupanda ndege ya Shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea jijini Mwanza. Shirika la
Ndege la Fastjet ni miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akiwa na 'crew'
iliyoambatana na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo
wakipanda ndani ya ndege ya Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa
wadhamini wa Jembeka Festival 2016 kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea
jijini Mwanza.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege na Mwanamuziki wa
Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya Shirika
la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016
mara baada ya kutua jijini Mwanza. Kampuni ya simu mkononi Vodacom
Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana
na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK
Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe
Media Group pamoja na Coca Cola.
Baadhi
ya wapiga vyombo waliombatana na msanii wa Marekani, Neyo wakishuka
kwenye ndege ya shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa jijini
Mwanza jioni. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio
wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la
Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security,
Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group
pamoja na Coca Cola.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla
(wa pili kushoto) na Mwanakamati ya Jembeka Festival 2016, Sharon
wakiwasili na katika uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii.
Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016,
Costantine Magavilla, Afisa Habari wa Jembe Media Group, Gsengo pamoja
na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege katika
picha ya pamoja.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka
Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP
Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo
Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
Msanii
huyo anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo kwa kupiga 'Live Music'
katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo msanii wa kimataifa kutoka nchini,
Diamond Platnumz, FID Q, Stamina, Mr. Blue, Ney wa Mitego, Maua Sama,
Rubby, Baraka Da Prince, Juma Nature, MO Music na wengine wengi
watapanda jukwaa moja na msanii Neyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269