Kiongozi
wa Kambi rasmi ya Upinzania na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe (MB)
akimuuliza swali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Kassim Majaliwa (MB) kuhusu hali ya uchumi nchini ambapo Waziri Mkuu
Mhe. Majaliwa alimhakikishia kuwa Serikali ipo imara katika kusimamia
ipasavyo uchumi wa nchi.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB)
akijibu maswali ya wabunge wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB)
akiwashukuru wabunge mara baada ya kumaliza kujibu maswali wakati wa
kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini
Dodoma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) akijibu swali bungeni
ambapo alisema kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na raia katika
kuhakikisha inakabiliana na biashara haramu ya Madawa ya Kulevya.
Waziri
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu akijibu swali bungeni ambapo alisema ambapo alisema
Serikali imetenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kuboresha Magereza
ya watoto pamoja na makao ya Wazee nchini.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.
Suzan Kolimba akijibu swali bungeni ambapo alisema serikali ipo katika
mazungumzo na serikali ya China kwa ajili ya kuboresha zao la Tumbaku.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akijibu
swali bungeni ambapo alisema Wizara imetenga Shilingi bilioni 3 kwa
ajili ya kuboresha hali ya Magereza nchini.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongea na
wabunge na kuviasa vyama vya siasa vyenye tabia ya kufukuza wabunge
kuacha hivyo kwani hatuwatendei haki wapiga kura na ni gharama kwa
serikali. Picha na Hassan Silayo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269