Mgombea
wa urais nchini Marekani Donald Trump akiondoshwa katika jukwaa na
maafisa wa usalamaMgombea wa urais wa Marekani kwa tikiti ya chama cha
Republican Donald Trump ameimarisha kampeini zake mjini Nevada licha ya
kisa cha usalama kilochobabisha walinzi wake kumuondoa jukwaani kwa
muda.
Wafuasi
wake wanasema walinzi wake walifanikiwa kumuondoa jukwaani licha ya hofu
kwamba kulikuwa na mtu aliyekuwa amejihami kwa silaha miongoni mwao.
Bw.Trump
alikuwa anakaribia kilele cha hotuba yake ndani ya ukumbi wa Reno
uliyojaa wafuasi wake, na ghafla kukatokea rabsha karibu na jukwaa.
Taharuki ilitanda mahala hapo kabla ya walinzi wake kufanikiwa kumuondoa.
Wafuasi wake waliyojawa na hofu walianza kukimbilia lango la kutoka nje wa ukumbi huo kufuatia madai ambayo hayakudhibitishwa
Polisi wamemkamata mtu mmoja kufuatia tukio hilo lakini akaachiliwa muda mfupi baadaye.
Mtu huyo hakupatikana na silaha kama ilivyodaiwa.
Huku
zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu,wagombea wote wawili
wameimarisha kampeini zao katika jimbo muhimu la Florida linalo na
umaarufu wa kuamua mshindi wa uchaguzi wa urais.
Kumekuwa na ongezeko la watu wa asili ya hispania wanaopiga kura mapema Florida na Nevada.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema huenda hatua hiyo ikamnufaisha Bi Clinton.
Trump amesema atazuru jimbo la Minnesota ambalo chama cha Republican hakijawahi kupata ushindi kwa zaidi ya miaka arobaini.BBC
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269