Breaking News

Your Ad Spot

Jan 4, 2017

KINANA AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM WILAYA YA MONDULI, JACOB NKOMOLA, LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo ameongoza mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Jacob Nkomola, yaliyofanyika Mtoni Kijichi, Temeke Dar es Salaam.

Katika mazishi hayo walikuwepo piaa viongozi wengine wa ngazi ya juu wa CCM, wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu. Ngemela Lubinza.

Nkomola ambaye alifariki juzi jijini Dar es Salaam, mwili wake ulitangulia kuagwa nyumbani kwake, Mtoni Kijichi na baadaye kupelekwa katika Kanisa la Kianglikana, Mtoni Kijichi kabla ya kuzikwa katika makaburi yaliyopo Kijichi  saa kumi jioni. Kuona mfululizo wa picha tangu kuagwa mwili hadi maziko, tafadhali/>BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages