Naibu
waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwa na Mkuu wa
Magereza kamishna Juma Malewa akizungumza jambo na waanddishi wa habari
katika gereza la Ukonga Jijini Dar es salaam.
.Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo na
Mratibu wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza Bw. Julious Chege katika
gereza hilo la Ukonga,jijini Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo na
Kaimu kamishna wa Jeshi la Magereza Juma Malewa mara baada ya kukagua
Kiwanda cha kutengeneza Samani Katika gereza la Ukonga.
Na Anthony John Glob Jamii.
NAIBU
Waziri mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni amelitaka jeshi la
zimamoto na Uhamiaji kutoshona sare zao za uraiani, badala yake
wakashone katika jeshi la Magereza ili kubana matumizi ya serikali.
Masauni
ameyasema hayo leo katika ziara yake ya kutembelea Magereza
Ukonga,jijini Dar, ambapo amekagua Kiwanda cha Magereza
kinachojishughulisha na ushonaji wa nguo za wafungwa na nguo za askari
Magereza.
Sanjari
na hayo Mhandisi Masauni ametoa wito kwa Watanzania kwa kununua bidhaa
mbali mbali zinazo tengenezwa na jesi la Magereza ili kuunga mkono kwa
kazi nzuri wanazozifanya.
Aidha
amewapongeza askari wa jeshi la Magereza kwa kujitolea kujenga nyumba
zao bila kusubiri serikali kuwajengea na kuwaahidi kuwa Serikali
itaandaa bajeti Mwakani ili kumalizia maeneo machache yaliyo baki.
Naye
kaimu Mkuu wa Magereza Kamishina Msaidizi . Juma Malewa amesema Jeshi
hilo linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi kama mashine za kushonea
nguo, na mashine za za ufundi selemala , ukosefu wa mtaji wa kuendesha
shughuli za kilimo, hivyo amesema pindi serikali itakapo wawezesha
watajitosheleza kwa chakula na mahitaji mengine
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269