Breaking News

Your Ad Spot

Feb 3, 2017

BARAZA LA TATU LA WAFANYAKAZI MOI LAFUNGULIWA

MOI1
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MOI Prof, Bakari Lembariti akihutubia wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi wa Kikao cha Tatu cha Baraza Hilo, kutoka kulia ni Naibu Katibu Baraza la Wafanyakazi hilo, Mwenyekiti wa Tughe na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt, Othman Kiloloma
MOI2
Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt Othman Kiloloma akiwasilisha ripoti ya Utendaji ya Mwaka 2015/2016, 
MOI3
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Prof, Bakari Lembariti
MOI4
Makamu mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi MOI Prof , Bakari Lembariti akimkabidhi cheti Mfanyakazi bora wa Taasisi ya  MOI kwa  Mwaka 2015/2016 Rbert Ojock na pesa TSH. mil. 4(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MOI Profesa Bakari Lembariti jana amezindua kikao cha Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa MOI katika ukumbi wa IDDI NYUNDO katika halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam. kikao  kimehudhuriwa na zaidi ya wajumbe 50 kutoka katika kila idara, vitengo na chama cha wafanyakazi wa MOI (TUGHE) na wajumbe wa TUGHE mkoa.
Akizindua Baraza hilo Profesa, Lembariti alisema anampongeza Mh, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Alisema ” Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini MOI Mh. Zakia Meghji natumia Fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli kwa uongozi wake uliotukuka na jitihada zake za kuboresha huduma za afya hapa nchini, sote ni mashahidi“.
Aidha, Profesa Lembariti aliwakumbusha wafanyakazi wa MOI kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma ili kujenga imani kwa watanzania walio wengi ambao wanaitegemea MOI kama Taasisi pekee inayotoa Tiba ya kiwango cha juu cha rufaa kwenye Tiba ya Mifupa, upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.
Pia Profesa, Lembariti alisema ni vyema wajumbe wa Baraza la MOI wakatumia vikao vya Baraza kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili Taasisi ya MOI na kutafuta muarobaini  ili Taasisi ya MOI iendelee kutoa huduma bora,
Kwa upande mwingine Profesa,  Lembariti aliwakabidhi zawadi wafanyakazi Bora wa MOI kwa mwaka 2015/2016 ambapo, Robert Ojock na pesa TSH. mil. 4 aliibuka kidedea na kuwa mfanyakazi Bora wa MOI na kujipatia cheti na fedha taslimu kiasi cha Tshs Milioni 4, nafasi ya pili ikishikwa na Bwana Lucas Machage akijipatia cheti na kiasi cha Tshs Milioni 2 na nafasi ya tatu ikishikwa na Bi Betty Shila ambaye alijipatia  cheti na kiasi cha Tshs Milioni 1.5
Kwa upande wake ,akiwasilisha ripoti ya utendaji wa Taasisi ya Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt. Othman Kiloloma alisema kutokana na ongezeko kubwa la ajali ambazo zimepelekea ongezeko kubwa la wagonjwa MOI, Taasisi ya MOI iko kwenye mpango mkakati kabambe wa kushirikiana na baadhi ya hospitali za rufaa za pembezoni kwa kuwapeleka wataalamu kutoa huduma katika hospitali hizo na kupunguza kama si kuondoa kabisa wimbi la wagonjwa wanaopokelewa MOI
Dkt, Kiloloma alisema kwamba Taasisi ya MOI imeendelea kuwa Kitovu cha Weledi katika matibabu ya Mifupa , Ajali , Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati ambapo mwaka 2015 MOI ilitoa utafiti bora wa mfupa mrefu wa paja duniani ,ambapo utafiti uliwasilishwa katika Taasisi ya kimataifa ya upasuaji wa mifupa duniani  ya Marekani (AOTA)
Vilevile, Dkt. Kiloloma aliwaomba wajumbe wa Baraza la MOI kutoa michango yenye tija ili kupata matibabu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Taasisi ili Taasisi iendelee kutoa huduma bora kwa watanzania

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages