Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WASHINDI
wa bahati nasibu ya kampeni ya kuweka amana DCB inayojulikana kama
Boresha maisha na DCB wamekabidhiwa zawadi zao na Kaimu Mkurugenzi wa
Benki ya DCB Said Kapilima leo Jijini Dar es salaam.
Akizungumza
kabla ya kutoa zawadi kwa washindi hao, Kpilima amesema kuwa hii ni
droo ya pili ya bahati nasibu kwa wateja wa benki hiyo kunufaika na
kampeni ya kuweka amana kwa akaunti za Akiba binafsi, akaunti za watoto
na WAHI iliyoanza mwezi Novemba mwaka jana.
Kapilima
amesema kuwa, lengo kuu la kampeni hii ni kuboresha maisha ya wateja wa
benki hiyo kwa kuwapatia zawadi mbalimbali pindi mteja anapokuwa
anaweka fedha mara kwa mara na inawadsaidia kuongeza ukubwa wa amana na
kuwajengea utamaduni wa kujiwekea akiba benki kwa matumizi ,mengine.
Katika
droo ya pili iliyochezwa mbele ya mkaguzi kutoka michezo ya bahati
nasibu ya Taifa Bakari Maggid iliweza kutoa washindi wawili wa simu za
mkononi, washindi wa tatu wa fedha taslimu za ada na washindi ishirini
wa tshirt.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya DCB Said Kapilima akimkabidhi zawadi ya
simu Mercelina Haule wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa bahati
nasibu ya kuweka amana DCB inayojulikana kama Boresha maisha na DCB leo
Jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya DCB Said Kapilima akimkabidhi zawadi ya
fedha taslimu kwa ajili ya ada ya watoto, Ziada Haule wakati wa utoaji
wa zawadi kwa washindi wa bahati nasibu ya kuweka amana DCB
inayojulikana kama Boresha maisha na DCB leo Jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya DCB Said Kapilima akikabidhi zawadi za
Tshirt kwa wateja waliofanikiwa kushinda bahati nasibu ya kuweka amana
DCB inayojulikana kama Boresha maisha na DCB leo Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya washindi wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Benki
ya DCB Said Kapilima (katikati), Meneja mwandamizi wa benki na matawi
Haika Machaku(wa kwanza kulia) wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi
wa bahati nasibu ya kuweka amana DCB inayojulikana kama Boresha maisha
na DCB leo Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269