Rais
Mstaafu Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitembelea mabanda mbalimbali
katika maadhimisho ya miaka 25 ya Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii
(CSSC) yaliyofikia kilele siku ya tarehe 22/02/2017 katika ukumbi wa
Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
Rais Mstaafu Mzee Mwingi akiwa katika Banda la Elimu la "Life Oriented
Approach (LOA)" , njia ya ufundishaji wa Elimu ya awali, katika mradi
unaotekelezwa na Kanisa Katoliki katika Majimbo ya Arusha na Same
Mkuu
wa Shirika la "Pressures Blood" Tanzania Padre Chesco Msanga,
akimkabidhi zawadi ya picha Rais Mstaafu Mzee Mwinyi kama kumbukumbu
alipoifungua Hospital ya St. Gaspar Itigi inayoendeshwa na shirika hilo
Mzee Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC)
Rais
Mstaafu Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitoa hotuba yake katika siku ya
kilele ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 tangia kuanzishwa kwa Tume
ya Kikristu ya Huduma za Jamii Tanzania
Mzee
Mwinyi akitoa Cheti kwa Profesa Costa Mahalu, moja ya watu waliyotoa
msaada mkubwa wa masuala ya Sheria kipindi Tume hiyo ilipokuwa
inaanzishwa
Rais
Mstaafu wa Serikali ya awamu ya pili, Alhaji Alli Hassan Mwinyi,
ameipongeza Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC) kwa kutimiza
miaka 25 tangu ilipoanzishwa mwaka 1992. Akiongea katika maadhimisho
hayo, Mzee Mwinyi amesema kuwa Serikali imekuwa ikitambua na kuthamini
mchango wa makanisa na Taasisi za dini katika kuboresha huduma za Jamii.
“Nimefarijika
sana kwa kupata taarifa kuwa hadi kufikia Septemba 2016, hospitali za
Kanisa 87 na vituo vya afya 45, vimeingia Mkataba na Serikali katika
kutoa huduma za afya”, alisema Rais Mstaafu Mwinyi.
Katika
hatua nyingine, Mzee Mwinyi aliongeza kuwa kwa upande wake yeye amekuwa
mstari wa mbele kwa kuwaasa ndugu jamaa na marafiki zake na Watanzania
wote kwa ujumla, kutumia huduma zitolewazo na hospitali za kanisa kwa
kuwa wanatoa huduma bora, kwa kuzingatia upendo
“
Ikiwa mnaona kazi zinawazidia na mnafikia sehemu mnanung’unika kwa
kuzidiwa na kazi nyingi, basi ningesema mgomvi wenu ni mie. Maana
nawaambia ndugu na Watanzania wenzangu, kuwa huduma nzuri za afya
zinapatikana katika hospitali za Kanisa, kwa kuwa unahudumiwa kwa upendo
pamoja na tabasamu,” aliongeza Rais Mstaafu, Mwinyi.
Rais
Mstaafu Mwinyi alimuomba Rais wa Tume aendelee kupanua na kuboresha
huduma za jamii, kwa utaalamu na ubunifu huku akiwaasa watumishi wa
sekta hiyo, kutofanya kazi kwa mazoea. Aliongeza kuwa uamuzi wa
kuanzisha Tume hiyo ulikuwa ni wa busara sana kwa manufaa ya Watanzania
walio wengi.
Mheshimiwa
Rais Mstaafu pia aliongezea kuwa Tume imefanya kazi kubwa ya kutekeleza
majukumu na malengo yake, kwani kwa taarifa alizo nazo ni kuwa katika
sekta ya elimu, idadi ya shule za makanisa imeongezeka kutoka 350 mwaka
1997, na kufikia takribani 1000 mwaka 2016, wakati katika Afya kutoka
idadi ya taasisi za afya 500 mpaka 900 kwa sasa. Alipongeza kwa
mafanikio haya makubwa yaliyopatikana ndani ya miaka hii 25 ya utendaji
wa Tume.
Katika
hatua nyingine, ameiomba Tume kuendelea kushirikiana kwa ukaribu na
Serikali katika kuboresha uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya
rasilimali kwani ni chache na zinahitajika kutumiwa na Watanzania wengi
wenye uhitaji pia.
Tume
ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) ni chombo kilichoundwa na Baraza
la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania
(CCT) mwaka 1992 kwa dhumuni la kuratibu na kusimamia huduma za kijamii
zitolewazo na Taasisi za Makanisa husika za Elimu na Afya nchini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269