Ofisa
Habari wa Kampuni ya Jumia Travel, Geofrey Kijangwa (kulia),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,
kuhusu kampuni hiyo kuzindua huduma za ndege. Kushoto ni Meneja Mkazi wa
Kampuni hiyo, Fatema Dharsee.
Meneja Mkazi wa Kampuni hiyo, Fatema Dharsee akizungumza na wanahabari.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Jumia Travel imetangaza kuwa imezindua huduma za ndege kwa ajili ya
wasafiri, hatua ambayo itapelekea kutanua wigo wa huduma zake.
Uzinduzi huu unakuja kipindi ambacho Kilele cha Mkutano wa Pili wa Masuala ya Anga Afrika ukifanyika nchini Rwanda.
Kwa
sasa mtandao huo nambari moja kwa huduma za hoteli barani Afrika unatoa
huduma za ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na mashirika makubwa ya
ndege yakiwemo Precision Air, Kenya Airways, Rwandair Express, Qatar
Airways, Emirates, Ethiopian Airlines, South African Airways, KLM, Fly
Dubai, Turkish Airlines, Air Arabia, Air Seychelles miongoni mwa
nyinginezo.
“Hii
ni hatua nyingine kwetu sisi tukiwa tunalenga kuwa wakala unayeongoza
kutoa huduma za usafiri kwa njia ya mtandao Afrika, huku tukiwapatia
wasafiri huduma za kipekee. Pia ni mpango wetu wa kutengeneza sehemu
moja ya kukidhi huduma zote za usafiri ikitoa malazi, vifurushi vya
huduma, na tiketi za ndege, zote zikiwa zinapatikana sehemu moja, katika
jitihada za kurahisisha usafiri Afrika,” alisema Paul Midy - Afisa
Mtendaji Mkuu wa Jumia Travel.
Jumia
Travel itakuwa ikitoa huduma kwa kushirikiana na washirika tofauti
akiwemo Amadeus. “Huduma hii (ambayo kwa sasa inapatikana kupitia
travel.jumia.com/flights) inawawezesha wateja wetu kutafuta,
kulinganisha, na kufanya huduma pamoja na kukata tiketi za ndege
mtandaoni kwa urahisi moja kwa moja kupitia kampuni mbalimbali za
mashirika ya ndege duniani,” aliongezea Midy.
Uzinduzi
huu unaongezea orodha ya huduma kwa wateja wengi wa Jumia Travel ambazo
wanaweza kuzifanya wenyewe kwa ndani na nje ya nchi. Ikiwa ni 3% tu ya
sehemu ya usafiri wa anga duniani, Afrika inaonyesha uwezekano mkubwa wa
kukua miaka ijayo, hususani kutokana na kuongezeka kwa uhitaji wa watu
wa daraja la kati na kukua kwa uchumi wa Afrika.
“Jumia
Travel imedhamiria kuwekeza kwenye kwenye soko ambalo linachochea
maendeleo ya sekta ya ukarimu barani Afrika. Kwa Shirika la Usafiri wa
Anga la Kimataifa, (IATA) kutabiri ukuaji thabiti kwa 4.8% kwenye idadi
ya abiria barani Afrika ndani ya miaka 5 ijayo, hii inathibitisha
tulivyojizatiti kimikakati kwa kutoa huduma zisizo na ukomo kwa
wasafiri,” alimalizia Midy.
Naye
kwa upande wake Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee
ameendelea zaidi kwa kufafanua kuwa, “Uzinduzi wa huduma hii kwenye
mtandao wetu ni kukidhi haja ya muda mrefu ya wateja wetu waliokuwa
wakiulizia endapo tutaweka na huduma za ndege. Ilikuwa inawawia ugumu
kufanya huduma za hoteli kupitia Jumia Travel na kisha kukata tiketi za
ndege sehemu nyingine. Tunaamini huduma hii itafungua Tanzania duniani
na kuileta dunia Tanzania, yaani mtu anaweza akafanya huduma za ndani au
nje ya nchi kwa sehemu kama vile Dubai, India na Uingereza. Lakini pia
huduma hii itahamasisha ukuaji wa sekta ya usafiri wa anga nchini
kutokana na mfumo kurahisishwa.”
“Huduma
hii tuna uhakika kuwa itakuwa ni suluhisho kubwa kwa wasafiri ndani na
nje ya nchi. Kwa sababu, msafiri atakuwa na uhuru wa kuchagua huduma
aitakayo kutoka kwa shirika la ndege alitakalo papo hapo kutokana na
orodha itakayojitokeza. Inamaanisha kwamba Jumia Travel tulichokifanya
ni kuzileta huduma za usafiri wa anga kutoka kwenye mashirika tofauti ya
ndege kuja sehemu moja kama tulivyofanya kwa hoteli. Msafiri hatokuwa
na haja tena kuwasiliana na shirika la ndege au wakala bali yeye
mwenyewe kupitia mtandao wetu kwenye kompyuta, tabiti (tablet) au simu
anaweza kujihudumia,” alihitimisha Dharsee.
Hivi
karibuni kampuni hiyo ilizindua ofa za msimu wa sikukuu ili kuhamasisha
utalii wa ndani barani Afrika. Kwa kuhusisha huduma za ndege ndani
yake, Jumia Travel itaendelea kuunga mkono jitihada za kuzifikia sehemu
mbalimbali za Afrika na nyinginezo duniani, wakati huo huo ikiwa na nia
ya dhati ya kuendelea kutoa suluhisho la huduma kwa usafiri.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269