Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Idara
ya Uhamiaji. Mkataba huo ambao unalenga kuimarisha huduma mbalimbali za
Idara hiyo pia umeelekeza kuanzia sasa Hati za Kusafiria (Pasipoti)
zitatolewa kwa siku tano za kazi kwa watakaoomba Makao Makuu Dar es
Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa
siku zisizozidi kumi. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara
hiyo, Victoria Lembeli. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara
hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi).
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
akizungumza na wananchi (wateja) waliofika Makao Makuu ya Idara ya
Uhamiaji kabla ya Balozi huyo hajazindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja
ulioandaliwa na Idara hiyo. Simba alisema Mkataba huo unalenga
kuimarisha huduma za Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana
kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es
Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa
siku zisizozidi kumi. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo,
Kurasini jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(aliyevaa tai) akimsikiliza mteja aliyefika kupata huduma ya Pasipoti
Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam mara
baada ya Balozi huyo kuwauliza maswali wateja waliofika ofisini hapo.
Hata hivyo, wateja hao walisema wanapewa huduma nzuri na maafisa wa
Idara hiyo. Balozi Simba alizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ambao
unalenga kuimarisha utoaji wa huduma bora katika Idara hiyo. Katikati ni
Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
akizungumza na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini kabla ya
Balozi huyo kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ulioandaliwa na Idara
hiyo ambao unalenga kuboresha zaidi huduma zitolewazo na Uhamiaji ambapo
kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya
mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa
mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Uzinduzi huo
umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Watatu kushoto (upande wa pili) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara
hiyo, Victoria Lembeli.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(katikati), akimsikiliza Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria
Lembeli alipokuwa anatoa maelezo mafupi jinsi Watendaji wa Idara yake
walivyouandaa Mkataba wa Huduma kwa Mteja ambao Balozi huyo aliuzindua
Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Mkataba huo
unalenga kuboresha zaidi huduma zitolewazo na Uhamiaji ambapo kuanzia
sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja
kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani
watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(kulia), akimkabidhi Vitabu vya Mkataba wa Huduma kwa Mteja Kaimu
Kamishna Jenerali wa Idara Uhamiaji, Victoria Lembeli mara baada ya
Naibu Katibu Mkuu huyo kuzindua Mkataba huo katika Ofisi za Makao Makuu
ya Idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Mkataba huyo
unaelekeza kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara
baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia
Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269