Naibu
Spika wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongea
na Wabunge (hawapo pichani) pamoja na Waandishi wa Habari kuhusu
umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya leo katika Uwanja
wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Naibu
Waziri, Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia
Wambura (Mb) akiongea na Wabunge wenzake (hawapo pichani) kuhusu umuhimu
wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya ya miili pamoja na
matarajio ya Uzinduzi wa Mazoezi yanayotarajiwa kuzinduliwa na Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yatatangazwa hivi
karibuni.
Mbunge wa
Viti Maalum (CCM), Mhe. Ritta Kabati akiongea na Wabunge wenzake pamoja
na Waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya
kulinda afya ya miili wakati wa mazoezi ya pamoja kwa Wabunge hao
wanawake yaliyofanyika leo 03/02/2017 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Mbunge wa
Jimbo la Ilemela Jijini Mwanza (CCM), Mhe. Angeline Mabula akiongea na
Wabunge wenzake pamoja na Waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kufanya
mazoezi kwa ajili ya kulinda afya ya miili wakati wa mazoezi ya pamoja
kwa Wabunge hao wanawake yaliyofanyika leo Uwanja wa Jamhuri
mjini Dodoma.
Baadhi ya
Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa
wameongozana na Spika wa Bunge (wa pili kushoto) wakifanya mazoezi
(Jogging) ikiwa ni sehemu ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya
kuweka sawa miili, mazoezi hayo yamefanyika leo katika Uwanja
wa Jamhuri mjini Dodoma.
Add caption |
Baadhi ya
Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa
wakifanya mazoezi ikiwa ni sehemu ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili
ya kuweka sawa miili, mazoezi hayo yamefanyika leo 03/02/2017 katika
Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa pili kushoto) akifanya
mazoezi ya mwili ikiwa ni sehemu ya ya kuweka sawa mwili, mazoezi hayo
yamefanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
(Picha zote na Benedict Liwenga)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269