Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aliyefikisha miaka 93 wiki hii, leo
anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kufanya sherehe ya kifahari
itakayohudhuriwa na maelfu ya wanaomuunga mkono nje ya mji wa pili kwa
ukubwa nchini humo wa Bulawayo. Chama tawala, ZANU-PF kinaandaa sherehe
ya kiongozi huyo aliyeko madarakani tangu mwaka 1980 na utawala wake
ukiwa umegubikwa na ukandamizaji wa wapinzani, udanganyifu wa kura na
kuanguka kwa uchumi. Kiongozi huyo wa taifa mwenye umri mkubwa zaidi
duniani kwa sasa, amekuwa akisherehekea siku hii kwa wiki nzima, huku
kituo cha televisheni cha taifa kikimmwagia sifa kemkem na pongezi.
Sherehe hiyo inagharimu Dola Milioni 1, hatua iliyowaghadhabisha
Wazimbawe wengi kufuatia upungufu wa chakula unaoikabili nchi hiyo.
Kufanyika kwa sherehe hiyo katika shule ya Matobo kumewachukiza wakazi
wa eneo hilo kwa kile kinachoaminika kuwa wahanga wa machafuko dhidi ya
wapinzani chini ya utawala wake katika miaka ya 1980 walizikwa eneo
hilo.
Your Ad Spot
Feb 26, 2017
Home
Unlabelled
WASHIRIKA WA MUGABE KUSHIRIKI SHEREHE YA KUZAKIWA
WASHIRIKA WA MUGABE KUSHIRIKI SHEREHE YA KUZAKIWA
Share This
About khamisimussa77@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269