Yazindua mnara mpya
wa mawasiliano kata ya Mponde Tanga
- Airtel yapeleka mawasiliano kwa vijiji 16 mkoani Tanga
- Yataimarisha ulinzi na mawasiliano kwa jamii.
Tanga Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel imewafaidisha zaidi ya wakazi elfu kumi na nne waishio katika vijiji vya
Lushoto na Bumbuli kwa kuwapatia mawasiliano ya uhakika kupitia ushirika wao na
mfuko wa Maendeleo wa mawasiliano kwa wote UCSAF yaani Universal Communication
Services Fund.
Uzinduzi
wa mnara wa mawasiliano wa Airtel katika kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani
Tanga, umekuja ikiwa ni wiki moja toka Mfuko wa maendeleo wa Mawasiliano kwa
wote na Airtel walipozindua minara mingine mitatu mkoani Dodoma.
akiongea
wakati kuzindua mnara huo Meneja Mauzo wa Airtel Tanga John Nada alisema
"Airtel tumejipanga kuendelea kutoa mawasiliano ya uhakika hasa kwa
kipindi hiki ambacho TCRA wamezindua huduma ya kuwawezesha wateja kuhama mtandano akiwa na namba
ileile ikiwa hawapati huduma nzuri na za uhakika, hivyo basi kwa wakazi wa Balangai,
Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu,
Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre Airtel ndio mtandao wenu wa ukahika kwa sasa”
“tunawaomba
wakazi wote mtumie fursa hii ya mawasiliano kwa kuwa wabunifu zaidi, tumumieni huduma ya Airtel Money kwa kuwa pia mko mbali
na huduma za kibenki tumeni na kupokea pesa ili kuboreshe kilimo kwa kutumia
mawasiliano haya ya uhakika toka Airtel” alisisitiza Bw, Nada
Kauli
ya wananchi juu ya tatizo la mawasiliano
zilithibitishwa na diwani wa kata hiyo ,Mh Edwin Mahunda kwamba wakazi wa Kata hiyo walikuwa wakipanda juu ya miti na
kwenye vilele vya milima wakitafuta mawasiliano ili kufanya mawasiliano ya
kibiashara na mambo mengine ya kijamii.
“Tunawashukuru
sana Airtel na UCSAF kwa jitihada zao za kutuletea mawasiliano, mawasiliano
haya yatasaidia wakazi wa hapa kijijini na pia yatawasaidia wanaishio mbali na
hapa ili kuweza kufanya shughuli zao vyema, awali hali ilikuwa mbaya sana,
ilikuwa huwezi kupiga simu mpaka ufike sehemu yenye muinuko” alieleza Mh
Mahunda-Diwani
Diwani
huyo aliendelea kusema kuwa “ninawaahidi wadau wa mawasiliano Airtel na UCSAF
kwamba tutayalinda mawailiano haya na tutayatumia vyema ili kukuza shughuli za
maendeleo ya kijamii na uchumi wa Wilaya yetu ya Bumbuli Mkoani Tanga
Pamoja
na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimila na serikali pia Uzindunzi wa
mnara huo katika kijijii cha kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga
ilipambwa na ngoma na burudani za asili za vijiji hivyo ambazo huchezwa mara
kwa mara wanapokuwa na jambo la furaha kwa jamii zao.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269