Mkurugenzi wa IBRA Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake
Wajasiriamali Tanzania (VoWET), Maida Waziri akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo kabla ya Mgeni rasmi kuzungumza
Wanakikundi cha Vicoba Endelevu wakiwa wamesimama na bango lao katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani
Mkurugenzi wa IBRA Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake
Wajasiriamali Tanzania (VoWET), Maida Waziri aliyebebwa na baadhi ya
wanawake waliojawa na furaha baada ya kuelezea historia yake ya
mafanikio iliyowasisimua wengi katika uwanja wa Mwembe Yanga Jijini Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani
Mkurugenzi wa IBRA Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake
Wajasiriamali Tanzania (VoWET), Maida Waziri aliyebebwa na baadhi ya
wanawake waliojawa na furaha baada ya kuelezea historia yake ya
mafanikio iliyowasisimua wengi katika uwanja wa Mwembe Yanga Jijini Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza katika Maadhimisho Dar es Salaam leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Mwanahabari wa Mtembezi Blog akiwajibika
Akina mama katika muonekano pichani wakifatilia kwa umakini wakiwa na bango lenye ujumbe maalumu
Mwanahabari akidadisi jambo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Farijika Production, Nipael Kamwava inayo jishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa dawa mbalimbali za asili za Binadamu
Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), wakiwa katika picha ya pamoja katika Maadhimisho ya Wanawake Duniania
Baadhi ya wafanyakazi wanawake Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa kusherehekea siku ya Wanawake
Duniani kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam,
Machi 8, 2018.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Salma Omary akizungumza na wanahabari wakati wa Maadhimisho hayo alisema,
katika kuondoa changamoyo zinazo jitokeza katika kutatua maswala
mbalimbali, inahitaji sana ushirikiano wa wanawake wenyewe kwa wenyewe
na kujitabua kwamba wao ni akinanani ili waweze kuondoa hizo changamoto
kwa kukaa pamoja na kujadili kwa pamoja na ndipo kunaweza kupatikana
mafanikio, pia akitowa wito kwa akinamama wote kwa kujiamini, wasikate
tamaa na mahali amapo pana utata anachangamoyo nyingi za kutosha asisite
kuwaona wanawake wenzake kama, jumuiya za wanawake sehemu mbalimbali
kama vijijini na mijinina akasema kama sehemu za ibada na anaweza
kupeleka changamoto hizo zinaweza kupatiwa ufumuzi na hata kwa mawazo
kuliko kujifungia ndani na hatimaye kukata tamaa
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amevitaka vikundi vya VICOBA
kujisajili mapema iwezekanavyo ili vikundi hivyo viweze kutambulika na
kupata uwezeshaji kiuchumi.
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya, Lyaniva
ameeleza kuwa vikundi vya VIKOBA vilivyopo ni takribani 2748 lakini kati
ya hivyo vilivyosajiliwa na kutambulika ni 746, hivyo vikundi 2200
havijasajiliwa, hivyo ni vyema vikasajiliwa haraka iwezekanavyo ili
viweze kupata fursa hiyo adhimu ya uwezeshaji kiuchumi.
Lyaniva ameeleza kuwa Machi 20 mwaka huu kutakuwa na jukwaa la
uwezeshaji wanawake katika uwanja wa Mnazi Mmoja ambapo mgeni rasmi
atakuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu hivyo ni vyema wakajisajili mapema
wapate fursa hiyo,
pia amewaagiza Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
kuandaa programju ya mafunzo kwa wanawake ambayo itakuwa na tija ya
kuwaelimisha na baadae wataweza kujiajiri, hivyo programu hiyo
iwasilishwe kwa Mkuu wa Mkoa ndani ya mwezi mmoja.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa IBRA Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake
Wajasiriamali Tanzania (VoWET), Maida Waziri amewataka wanawake nchini
kujituma na kuwa wabunifu katika biashara zao jambo litakalo wapelekea
kufanikiwa, huku akisisitiza elimu na mtaji siyo chanzo cha kukata tamaa
bali kufanya kazi kwa bidii na kutumia taarifa sahihi zitakazo
wapelekea kufanikiwa kama ilivyokuwa kwake,
ambaye amefikia hatua ya
kupewa tuzo na Rais Mstaafu Jakaya Kikwetu kwa kuwa Mkandarasi bora
2011-2015.
Siku
ya Wanawake Duniani husherekewa Machi 8 kila mwaka, ambapo kitaifa
imesherekewa Mkoani Singida na mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, huku kauli
mbiu ikiwa Tanzania ya Viwanda Mwanamke ni Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269